BONDIA Fransic Cheka atapanda ulingoni kwa mara ya kwanza kabisaa baada ya kutoka jera ambapo atacheza na Kiatchai Singwancha kutoka Thailand.
Mpambano uho wa raundi kumi utafanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam, akizungumza matahalisho ya mpambano uho Promota Kaike Siraju amesema kuwa amejipanga vizuri kwani kila kitu kinaenda vizuri kwa ivi sasa ambapo mabondia wa utangulizi wote wanatarajia kusainishwa wiki hii.
Mpambano huo utakaosimamiwa na chama cha ngumi za kulipipwa nchini P.ST chini ya rais wake Emanuel Mlundwa wamesema kuwa wao wako tayali kwa mpambano huo na bondia wa Thailand ataingia nchini siku tatu kabla ya mpambano huo ambao uatavuta hisia za wapenzi wengi wa mchezo wa ndondi nchini.
Siku hiyo Vicent Mbilinyi 'Sugu' atavaana na Keis Amal Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez , Mike Tyson,Mohamed Ali, Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi.
Pia kutakuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.