ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 6, 2015

WAZIRI WA AFYA AKIRI NA KUSEMA BADO KUNA UGUMU KWA WANANCHI KUCHANGIA KATIKA AFYA

Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dr.Seif Rashid kulia akiwa na mwandishi mkongwe wa habari hii Victor Masangu wa kulia mara  baada ya kumaliza kufanya mahojiano maalumu. 
Na Victor Masangu, Pwani
SERIKALI imesema kwamba pamoja na kuongeza juhudi katika kuboresha sekta ya afya lakini bado kuna changamoto kubwa kwa wananchi kuwa na mwamko mdogo wa kujiunga katika mfuko wa afya ya jamii, hali ambayo inachangia kutotimiza malengo ya serikali katika kutoa huduma ipasavyo  husasan  katika upatikaji wa madawa.
 
Hayo yamebainsihwa na Waziri wa afya Dr, Seif Rashid alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi  katika mahojiano maalumu kuhusina na changamoto zinazowakabili katika sektaya afya pamoja na mikakati waliyojiwekea katika kukabiliana na hali hiyo .
 
 
Dr Seif ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji alisema kuwa kwa sasa wananchi wamekuwa na mwamko mdogo  sana wa kujiunga katika mfuko wa afya ya jamii kutokana na kutokuona umuhimu kwani pindi wanapoandikiwa dawa na daktari matokeo yake wanazikosa.
 
Akifafanua zaidia kuhusina na hali hiyo Dr Seif alisema kuwa kuwepokuwepo n aachangamoto hiyo ya baadhi ya wananchi wanapokwenda katika zahanati, au vituo vya afaya wanakosa huduma ya madawa hivyo inawalazimu kwenda kununua madukani wakati wamechangia hivyo wanakata tamaa.
 
“Ndugu mwandishi mimi nakiri kabisa kuwepo kwa changamoto hii ya wananci wengine kutokuwa na mwammko mkubwa wa kujiunga katika mfuko wa afya ya jamii, lakini kitu kikubwa ambacho mimi ninaweza kusena ni kutokana wananchi hao wanakata tama kutokana na kukosa huduma ambayo wanastahili kwani dawa ni kweli wakati mwingine hawapati kwa muda muhafaka,” alisema Dr Seif.
 
Aidha aliongeza kuwa katika kuhakikisha kwamba vituo vya afya na zahanati vinakuwa vinatoa huduma staili kwa wananchi wote wataweza mikakati kabambe ya kuhakikisha wanapeleka madawa katika sehemu husika ili kuweza kuondoa malalamiko ambayo ndio yamekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wananchi kijiunga katika mfuko wa afya ya jamii.
 
Alisema kwamba kwa sasa wananchi wanapaswa kubadilika na kuwa na mtazamo chanya wa kuweza kujitahidi kwa hali na mali kujinunga katika mfuko wa afya ya jamii kwani ni mkombozi mkubwa pindi wanapotapwa na amagonjwa mbali mbali inawapa fursa ya kutibiwa bure tofauti na mwananchi ambaye ajajiunga.
 
Alisema kwamba katika kukabiliana na changamoto hiyo ya upatikanaji wa madawa hususan katika maeneo ya vijijini ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakiisha kwamba michango yote amabyo inatolewa na wananchi inatumika katika matumizi sahihi ya ununuzi wa madawa na sio vunginevyo ili kuweza kuondokana na lawama amabzo zimekuwa zikitolewa.
 
Katika hatua nyingine alisema kwamba serikali itajitahidi kuimarisha miundombinu ya majengo kuanzia zahanati, vituo vya afya vyote, pamoja na hospitali lengo ikiwa ni kuboreshaa huduma ya afya kwa wananchi wote ambao wanakwenda kupatiwa huduma sambamba na kusimamia upatikanaji wa madawa bila ya kuwa na ubaguzi wowote.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.