ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 6, 2015

AIRTEL YAKABIDHI VITABU VYA SAYANSI KWA SHULE YA SEKONDARI YA King'ongo DAR ES SALAAM

Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akionyesha sehemu ya vitabu kabla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya milioni 4/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Shule ya Sekondari ya King’ongo iliyopo Kimara katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Waliokaa (kutoka kushoto) ni Meneja wa Airtel Tawi la Kinondoni, Fadhili Mwasyeba, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo, Godfrey Mheluka na Mkuu wa Shule hiyo, Nyaibuli Bhoke.
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kushoto), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya milioni 4/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya King’ongo, Godfrey Mheluka katika hafla iliyofanyika shuleni hapo Kimara jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel Tawi la Kinondoni, Fadhili Mwasyeba (kushoto) na Mkuu wa Shule hiyo, Nyaibuli Bhoke (wa pili kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya King’ongo, Godfrey Mheluka (kulia), akikabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya milioni 4/-, kwa Mkuu wa Shule hiyo, Nyaibuli Bhoke baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ katika hafla iliyofanyika shuleni hapo Kimara jijini Dar es Salaam jana.
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kushoto), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya milioni 4/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya King’ongo, katika hafla iliyofanyika shuleni hapo Kimara jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia (kutoka wa pili kushoto)ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Godfrey Mheluka, Afisa Elimu na Takwimu wa Manispaa ya Kinondoni, Omary Ahmed na Mkuu wa Shule hiyo, Nyaibuli Bhoke .
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya King’ongo wakifurahia vitabu vya masomo ya sayansi, baada ya Kampuni ya Airtel kupitia Mradi wake wa  ‘Airtel Shule Yetu’ kukabidhi vitabu vyenye thamani ya milioni 4/- kwa shule hiyo katika hafla iliyofanyika shuleni hapo Kimara jijini Dar es Salaam jana.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya King’ongo wakifurahia vitabu vya masomo ya sayansi, baada ya Kampuni ya Airtel kupitia Mradi wake wa  ‘Airtel Shule Yetu’ kukabidhi vitabu vyenye thamani ya milioni 4/- kwa shule hiyo katika hafla iliyofanyika shuleni hapo Kimara jijini Dar es Salaam jana.

Airtel yakabidhi vitabu vya sayansi kwa Shule ya Sekondari ya King’ongo  Dar es Saalam.
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imetoa msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa Shule ya Sekondari ya King’ongo iliyopo Kimara katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Vitabu hivyo vyenye thamani ya shilingi million 4 vilitolewa na Airtel chini ya mradi wa Airtel shule yetu lengo likiwa nikusaidia kutatua uhaba wa vitabu mashuleni na kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule za sekondari nchini.

Akiongea wakati wa halfla ya kukabithi vitabu Meneja huduma kwa jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi alisema “ Tangu mradi uanze takribani miaka 10 iliyopita tumeweza kuzifikia shule nyingi hususani shule zenye uwiano wa wasichana wengi zaidi. Tunaamini mradi huu utaendelea kuwawezesha wanafunzi wengi kupata nyenzo za masomo nakuwapatia motisha wasichana kujiunga na masomo ya sayansi na kuwaendeleza zaidi kielimu kwani tunatambua tukimuwezesha mwanamke tumewawezesha jamii kwa ujumla.

Tunatoa wito kwa wanafunzi kuvitumia na kuvitunza vitabu hivi vizuri ili viweze kutoa tija kwa wanafunzi waliopo na watakao jiunga na shule hii, tunaahidi kuendelea kuziwezesha shule nyingi zaidi kupata vifaa muhimu vya masomo kwa njia za kielectronikia kwa nji ya mtandao mkakati utakaotambulishwa hivi karibuni.

Aidha Airtel kupitia wafanyakazi chini ya mpango wake wa Airtel tunakujali bado pia wanaendelea na mkakati wakusaidia maendeleo ya shule mbalimbali nchini. Chini yamradi wake wa Airtel Tunakujali shule mbalimbali ikiwemo shule ya ushindi jijini Dar esa saalam zimefaidika kwa kufanyiwa ukarabati wa darasa la awali shule.  Sambamba na hilo shule ya watoto wenye mahitaji maalumu ya pongwe mkoani tanga nayo imepata msaada wa kujengewa darasa ambalo linategemea kukabithiwa rasmi mwisho mwa mwezi huu kupitia Airtel Tunakujali.

Miradi hii yote ya Airtel Shule yetu na Airtel Tunakujali inalengo la kuziwezesha jamii zinazotuzunguka kuwa na mazingira bora yatakayowezesha utoaji wa elimu bora kwa watanzania na jamii kwa ujumla.Aliongeza Bayumi.

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari ya King’ongo Nyaibuli Bhoke alisema “ tunawashukuru sana Airtel kwa kuleta msaada huu wa vitabu shuleni hapa, shule yetu imekuwa na upungufu wa vitabu hivyo msaada huu umekuja kwa wakati muafaka. Natoa wito kwa wanafunzi kuvitumia vizuri vitabu hivi kwa kuvisoma ili viweze kuongeza ufaulu shuleni hapa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.