ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 10, 2015

WAZIRI KABAKA AMALIZA MGOMO WA MADEREVA.

Waziri wa kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amekutana na uongozi wa juu wa Madereva wa vyombo vya usafirishaji nchini na amefanikiwa kumaliza mgomo wa madereva hao baada ya kufuta agizo lililokuwa likiwataka madereva wa maroli na mabasi kwenda kusoma tena katika Chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT) (PICHA NA MAKTABA)

Kuhusu suala la madereva kusoma, Serikali na madereva wamekubaliana kukutana mwezi huu tarehe 18 kuzungumza njia mbadala ya kutumika.

Miongoni mwa malalamiko ya madereva ilikuwa ni kukerwa n atochi za barabarani, hivyo jeshi la polisi wamekubali kuziondoa.

Pia Serikali imeagiza madereva wote wapewe mikataba ya ajira za uhakika na waajiri wao na trafiki wameagizwa kulifuatilia hilo. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.