Wamiliki wa mabasi kupitia madereva wao wamegoma kutoa huduma za usafiri hivyo hakuna basi linaloingia au kutoka mjini hapa.
Mamia ya abiria wamekumbana na adha na usumbufu mkubwa wasijue nini hatma yao kwa kushindwa kusafiri asubuhi ya leo.
Akina mama, akina baba pamoja na watoto wao wameendelea kurandaranda huku na kule wakihaha kupata taarifa nini hatma yao na wala wasipate mtoa taarifa sahihi.
Wananchi wanaoishi mbali hawajajua kama wanasafiri au laa na kama watabaki nani atawawezesha au wapi pa kujisitiri.
Wazee na wagonjwa ambao wanao hitaji kusafiri kwenda mikoa mingine either kwaajili ya kupata matibabu au kurejea makwao mara baada ya kupata tiba toka vituo mbalimbali vya afya ikiwemo hospitali ya Rufaa Bugando wameshindwa kuondoka ndani ya muda muafaka na hata wasijue hatma yao na nani atakaye wahudumia.
Sababu kuu za mgomo huu kwa juu juu zinatajwa kuwa zinatokana na sheria zilizowekwa kuanzia suala la udhibiti mwendo ambapo wanapaswa kuendesha mwisho speed 80 na si juu ya hapo, mwendo unao walazimu either kuchelewa kufika au kulala njiani na si kufika siku hiyo hiyo kwa safari za mbali.
Leseni walizonazo madereva hao wa mabasi hazitambuliki wanaambiwa wakasome leseni zote walizonazo ni feki,hivyo zikimaliza muda wake wanapaswa warudi darasani ambapo gharama ya masomo ni shilingi laki 560,000/= kutoka gharama ya awali ambayo ilikuwa shilingi 200,000/=
"Kama walijua watagoma si wasinge tukatia tiketi...." Ilisikika sauti ya abiria huyu.
Msururu wa mabasi yaendayo wilayani, maeneo mbalimbali hapa nchini na pengine hata nje ya nchi kwa nchi jirani... kuna basi linalotoka.
Hata kama yakiruhusiwa vipi msongamano huko barabarani? Vipi kwa safari za mbali? Na vipi kuhusu mwendo kuna utaratibu gani kudhibiti? Hivi kwa mpango huu haturudi kule kule kwenye ajali? Busara inahitajika.
Yote hayo yakiendelea hakuna tamko lolote lililotolewa na Mamlaka husika ya Usafiri wa Majini na nchi Kavu SUMATRA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.