ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 9, 2015

OBAMA APINGA UBADILISHAJI WA MAUMBILE

Mwanamume aliyebadilisha maumbile na kuwa mwanamke
Rais Barrack Obama amesema swala la kisaikolojia miongoni mwa vijana ili kubadilisha maumbile yao linafaa kukoma mara moja.
Wengi wa wanaotaka kufanyia mabadiliko ya maumbile yao ni watu wa mapenzi ya jinsia moja hasa vijana.
Mshauri mkuu katika Ikulu ya Marekani Valerie Jarrett amesema kuwa utawala wa Bwana Obama umekubali kwa kauli moja kuwa ushahidi wa kisayansi kuhusiana na maamuzi ya kujibadilisha maumbile, ni swala ambalo haliwezi kukubalika kitaaluma na kimatibabu.
Taarifa hiyo ya Obama inajiri baada ya kifo cha kijana mmoja ambaye alikuwa amebadili jinsia yake na ambaye alijitia kitanzi mwezi wa Disemba baada ya kulazimishwa kuhudhuria mabadiliko hayo ya kimaumbile.
KUTOKA CHINA.
Kijana wa miaka 25 kutoka Guangzhou nchini China mnamo mwaka 2013 alifanyiwa oparesheni ya kujibadili maumbile na kuwa mwanamke kwa asilimia 100.

Akijulikana kwa jina la Alias, Xiao Xiang, jamaa huyo anasema tangu akiwa mvulana alipenda sana vitu vya kike sanjari na kuvaa sketi fupi ile hali akiwa mwanamme hivyo ana kiu kubwa kuona mwili wake unakamilika na kuwa full wa kike.

Cha kustaajabisha zaidi na chakustusha ni kuwa jamaa anapenda wanaume kinoma.
Kisaikolojia jamaa anapenda kuwa binti.

Miezi sita baadaye, jamaa aliendelea kufanyiwa surgeries upande wa uso na maumbile yake ya siri ili kukamilisha muonekano wake kuwa wa kike kamili.

Anasema kuwa alipata wazo kuwa mwanamke tangu akiwa na umri wa miaka 16. Miaka miwili iliyopita akaanza kutembea mitaani akiwa ametinga mavazi ya kike.

Mungu kiepushe kizazi chetu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.