ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 30, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AREJEA NCHINI BAADA YA KUHUDHURIA MKUTANO WA DHARURA WA SADC, JIJINI HARARE, ZIMBABWE, MUGABE AKABIDHI RASMI CHUO CHA UTUNZAJI AMANI

R1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wenzake walioshiriki katika Mkutano wa dharura wa SADC, mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo kwenye Hoteli ya Rainbow Jijini Harare, Zimbabwe, jana Aprili 29, 205. Makamu wa Rais amerejea nchini jana kuendelea na majukumu ya Kitaifa. Picha na OMR
R2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na baadhi ya viongozi wenzake wakitoka kwenye ukumbi wa mkutano baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa dharura wa SADC jana. Picha na OMR
R3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya Zimbabwe, huku akipunga mkono kuaga wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Zimbabwe jana Aprili 29, 2015 kurejea nchini. Kushoto kwake ni mkewe mama Zakhia Bilal. Picha na OMR
R4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Adadi Rajab, wakati akiondoka kurejea nchini baada ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC, jijini Harare, Zimbabwe jana April, 29, 2015. Picha na OMR
R6
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akimkabidhi Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt Stargomena Tax, mfano wa funguo kama ishala ya makabidhiano ya Kituo cha Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, wakati wa Mkutano wa dharura uliofanyika jana Aprili 29, 2015 kwenye Hoteli ya Rainbow jijini Harare, Zimbabwe.
Kufuatia makabidhiano haya, Chuo hiki sasa kitakuwa kinamilikiwa na SADC na matumizi yake yatahusisha vyombo na wataalamu mbalimbali wanaohusika na masuala ya utunzaji amani ndani ya nchi hizi, ili kupata mafunzo ya kuboresha kazi zao kufuatia migogoro kuwa mingi katika nchi mbalimbali Afrika. Picha na OMR 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.