Na Victor Masangu, Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo amewataka wazazi na jamii kwa ujumla kuachana na imani potofu kwamba ukipatiwa chanjo madhara na badala yake wahakikishe wanabadilika na kuwa na mtazamo chanya wa kuwapeleka watoto wao kupatiwa kinga hiyo kwa lengo la kuwalinda watoto wao wasiambukizwe na milipuko ya magonjwa mbali mbali.
Ndikilo ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya chanjo katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani katika sherehe ambazo zimefanyika katika kituo cha afya Mlandizi.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alibainisha kuwa katika Mkoa wa Pwani kumekuwepo na baadhi ya wazazi na walezi hawataki kuwapeleka watoto wao kupatiwa chanjo kwa madai kwamba zina madhara kwa binadamu kitu ambacho amedai sio cha kweli na kwamba waachane na kupotosha jamii kwani chanjo hiyo inasaidia kupunguza vifo vya watoto.
Alisema kwamba kwa sasa wazazi na walezi wanapaswa kubadilika na kuhakikisha kwamba wanawapeleka watoto wao katika kupatiwa chanzo ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiwango kikubwa katika kuwalinda na malazi mbali mbali kama vile polio na mengineyo.
"Kikubwa mimi napenda kuwahasa wananchi wote wa mkoa wa pwani kuacahana kabisa na imani potofu na badala yake sasa wabadilike na kuangalia umuhimu wa chanjo hizo ambazo zinatolewa kwa watoto wote ambao wana umri wa chini ya mika mitano hivyo ombi langu ni kwenda katika maeneo ambayo yametengwa ili watoto wote wanaostahili waweze kuapatiwa chanjo hiyo," alisema Ndikilo.
Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu wa kituo cha afya mlandizi Witness Mulegi alisema kuwa umuhimu wa kupatiwa chanjo hiyo hususan kwa watoto kunasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa mbali mbali ambayo yanaweza kuzuilika kwa kupatiwa chanjo.
Nao wakinamama ambao walihudhuria katika uzinduzi huo akiwemo Jenipher Alaulensi pamoja na Fatma Shaban wamesema kwamba zoezi hilo la kupatiwa chanjo kwa watoto wao lina umuhimu kwani linawasaidia kwa kiasi kikubwa kuwalinda watoto wao kutopata mlipuko wa magonjwa.
Naye mratibu wa huduma za chanjo katika Mkoa wa Pwani Abasi Ncha alisema kwamba kwa sasa wapo katika mikakati kabambe ya kutoa elimu juu ya umuhimu wa kupatiwa chanjo kwa watoto pamoja na kuwenda kutoa semina mbali mbali hususan katika maeneo ya vijijini.
Katika maadhimisho hayo watoto wapatao 115 wenye umri wa chini ya miaka mitano katika halmashauri ya Wilaya ya Kibaha,Mkoa wa Pwani wanatarajiwa kupatiwa chanjo,ambao walibainika kutopatiwa chanjo katika awamu ya kwanza kutokana na kuwepo kwa mwamko mdogo kwa wazazi na walezi sambamba na kuwepo kwa imani potofu kuwa chanjo hizo wanazopatiwa zinamadhara.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.