ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, April 29, 2015

KUELEKEA MAANDALIZI YA KILELE CHA MEI MOSI RAIS KIKWETE KUTUA MWANZA KESHO.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akizungumza na wafanyakazi wa sekta mbalimbali hii leo ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa maonesho ya Mei Mosi 2015 ambapo kitaifa kwa mwaka huu yanafanyika jijini Mwanza, Siku ya Ijumaa (katika maadhimisho ya Mei Mosi) Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmikwenye uwanja wa CCM Kirumba.   
BOFYA PLAY MSIKILIZE MKUU WA MKOA.
Licha ya miundo mbinu kuwa katika hali tete kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wafanyakazi na wahudumu toka makampuni na mashirika mbalimbali hawajasita kujitokeza.
Msikilize msemaji huyu toka SUVRE wadau wanao jishughulisha na uuzaji wa vifaa na utoaji huduma za usalama wa mfanyakazi maeneo ya kazi. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.


Mabanda na hili ni banda la Bima.
Ushauri na upimaji afya bure unazingatiwa viwanjani hapa.
Watu wameweka kambi viwanjani hapa.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umewekeza ndani ya viwanja hivi.
Upimaji, ushauri, na huduma ya kwanza inafanyika ndani ya banda hili la Bima ya Afya kwenye viwanja hivi vya Furahisha hapa jijini Mwanza.
Ushauri wa kina.
Gari mahususi kwa akinamama wajawazito waliochelewa kuwahishwa cliniki katika zama za kujifungua au wenye uhitaji wa dharula.
Wakali wa digitali 'Startimes' nao wamejikita humu.
Banda la Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Mwanza (MWAUWASA).
Taswira toka mbali viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
Barua toka Posta.
Usalama kazini hususani sekta ya Kilimo.
Anglo Gold Ashanti Geita Gold Mine na banda lao.
Ukaguzi wa kamati ya Maonesho ukifanyika kupita banda baada ya banda ukitoa maksi maandalizi kuelekea kilele ambapo kutakuwa na ugawaji tuzo...zitakazotolewa na Mhe.Rais Jakaya Kikwete. 
Ufafanuzi toka banda la TANROADS MWANZA.
Moja kati ya madaraja yalojengwa na TANROADS jijini Mwanza ni daraja hili la Mabatini (kama linavyo onekana pichani).


Taswira ya viwanja vya Furahisha Mwanza jioni hii.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.