SIMIYU: Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu linawashikilia askari wawili wa Jeshi la Magereza na Polisi kwa kukutwa na noti bandia ikiwa pamoja na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Charles Mkumbo alisema kuwa askari hao walikamatwa juzi saa 9 mchana katika mtaa wa Old Maswa kata ya Nyakabindi Wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Alisema kuwa askari hao walifika kwenye Kibanda cha M-pesa kinachomilikiwa na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Old Maswa, Kassian Luhende (29) wakiwa na pikipiki yenye namba za usajili T 403 CXW aina
ya Sunlg kwa lengo la kuweka fedha hizo kwenye akaunti yao ya simu.
Alisema wakiwa kibandani hapo walitoa noti 100 ambazo kama zingekuwa fedha halali zingekuwa na thamani ya Sh milioni moja na baada ya kuzishika alizitilia shaka na baada ya kuzikagua zaidi alizigundua hazikuwa halali.
Kamanda Mkumbo alieleza kuwa baada ya kugundua fedha hizo ni feki alichukua jukumu la kuwajulisha majirani zake ili kuomba msaada hivyo kuwakamata watu hao ambapo mmoja alijitambulisha kama dreva wa bodaboda.

“Baada ya wananchi kubaini mmoja alikuwa askari waliwatilia shaka zaidi ambapo waliweza kutoa taarifa Kituo cha Polisi Bariadi na ndipo askari walifika eneo la tukio na baada ya upekuzi tuliweza kubaini watu hao walikuwa ni askari, mmoja akiwa polisi na mwingine magereza,” alisema.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni askari mwenye namba H 2420 PC Seleman Juma (25) ambaye ni askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Mkoani Simiyu, askari namba B.6499 WDR Edmund Masaga (28) ambaye ni askari Magereza wilayani Bariadi.
“Baada ya askari hao kukamatwa mmoja wao PC Selemani Juma alipopekuliwa katika mfuko wa suruali yake alikutwa na noti zingine za Bandia za Sh 10,000 ambazo kama zingelikuwa halali zingelikuwa na thamani ya Sh 920,000 hivyo kufanya jumla ya noti walizokamatwa nazo kuwa 192. Askari huyo alipokwenda kupekuliwa nyumbani kwake alikutwa na sare za JWTZ ambazo ni Kaptura 4, Fulana 2, Sare pea 1 na Kitambaa cha JWTZ,” alisema.
Kamanda Mkumbo alisema uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa usambazaji wa noti bandia ndani ya mkoa huku akieleza kuwa mara baada ya uchunguzi kukamilika askari hao watachuliwa hatua za kinidhamu kwa kushtakiwa kijeshi na kisha kufikishwa mahakamani.

Alitoa onyo kwa askari Mkoani hapa kuacha tamaa ya pesa na badala yake walizike na ajira zao zinazowapatia pesa halali, huku akieleza kuwa kwa atkayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria na nidhamu.CHANZO: www.mabadiliko.com
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.