MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA ILALA, JERRY SILAA, ATOA MAGARI KWA WASHINDI WA AIRTEL YATOSHA ZAIDI
Dar es Salaam,
MSTAHIKI Meya wa Ilala, Jerry Silaa, ametoa magari kwa washindi saba wa promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi promosheni inayoendeshwa na Airtel maalum kwa wateja wa bando za Yatosha Zaidi.
Katika hafla hiyo ya kuvutia iliyofanyika makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam, wahudhuriaji walishuhudia washindi hao waliotangazwa Ijumaa wiki iliyopita wakiondoka na magari hayo mapya aina ya Toyota IST, kwa sababu tu walijiunga na bando za Yatosha Zaidi inayotolewa na Airtel Tanzania.
Washindi hao ni mamalishe mkazi wa Dar es Salaam, Sakina Mshamu Libwana, mganga wa tiba asilia kutoka Katavi Said Mashiko, tandiboi wa mabasi mkazi wa Tabata Justin William, Edson Mwansasu (mkulima, Kyela), Hamim Yoyo (mfanyakazi wa saluni, Korogwe, Tanga) na Ester Mashauri, muuguzi wa Hospitali ya Bugando, Mwanza.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mstahiki Meya Silaa alisema: “Ninafarijika sana kuona Watanzania kutoka kada mbalimbali wakiibuka washindi wa promosheni hii. Hii inaonyesha ni namna gani Airtel wamejipanga kuboresha maisha ya Mtanzania mmoja mmoja.
“Kingine kilichonifariji kwa leo ni kuona miongoni mwa washindi, wapo pia wakazi wa Manispaa ya Ilala ambako mimini ni Meya wao. Lakini, pongezi zangu ni kwa washindi wote nikiwaomba wasiache kutumia huduma za Airtel wao na jamaa zao.”
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso, alisema: “Kwa jinsi zawadi hizo zilivyosambaa nchini ni alama ya kuenea kwa uhakika kwa mtandao na huduma za Airtel Tanzania. Kwa magari haya 10 tu ya mwanzo, tayari tumepata washindi kutoka kila kona ya nchi, hii inafurahisha sana!”
Nae mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Airtel, Jackson Mmbando, alisema: “Ninachowasihi wateja wetu ni kuendelea kujiunga na huduma ya Airtel Yatosha Zaidi. Pia wateja wasizime simu zao za mkononi au kusita kupokea hasa kwa siku za Ijumaa kwani kila Ijumaa jioni, droo hii huchezeshwa.”
Mmoja wa washindi hao, aliwaambia waandishi wa habari: “………
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.