ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 23, 2015

MHESHIMIWA ANGELA KAIRUKI AHITIMISHA RASMI MKUTANO WA KIKANDA

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MHESHIMIWA ANGELA KAIRUKI AHITIMISHA RASMI MKUTANO WA KIKANDA

Dar es Salaam, JumapiliFebruari 22, 2015 Mkutano wa kikanda juu ya ukuaji na maisha ya baadae ya miji ya Afrika mashariki ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI INSTITUTE) umefungwa rasmi leo na Naibu waziri wa Nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.  Angela Kairuki katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.

Mkutano huo wa siku mbili uliohudhuriwa na wawakilishi wa ngazi za juu kutoka serikalini, mashirika ya kikanda na kimataifa, miji mikubwa, wasomi, sekta binafsi na asasi za kiraia umeweza kujadili na kuainisha mipango kabambe katika kutatua changamoto mbalimbali za ukuaji wa miji na jinsi gani tungependa kuishi mwaka 2050.
“Tatizo la ukuaji wa miji ni moja ya changamoto katika ukanda wa Afrika mashariki na nchi kwa ujumla. Ninaimani kuwa mkutano huu umeweza kujadili changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo kama nchi na ukanda mzima wa Afrika mashariki” alisemaMhe.Kairuki.

Aliongeza kuwa matatizo ya foleni na kubanana kwa makazi ni kutokana na mipangilio mibovu ya nyumba na makazi jijini Dar es salaam. Hivyo basi kwa kutatua changamoto hizi wakazi wa Dar na wa miji mbalimbali ya Afrika kwa ujumla wataweza kufurahia mahitaji yao muhimu na kuongeza kasi ya maendeleo.
Mhe. Kairuki pia aliweza kutambua mchango mkubwa wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI INSTITUTE) kwa kuleta mijadala yenye tija yenye lengo ya kustawisha uongozi bora na maendeleo kwa nchi za Afrika na dunia kwa ujumla.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa UONGOZI Institute, Prof. Joseph Semboja aliwashukuru watoa mada na washiriki wote walioweza kufika na kuhakikisha kuwa mkutano huu unafana.
“Lengo kuu la mkutano huu limekuwa ni kujadili juu ya ukuaji na maisha ya baadae ya miji ya Afrika na tumekubaliana wote kuwa ili haya yaweze kutimia ni lazima basi miji iongeze nguvu ya ukuaji wa uchumi ili kuongeza ajira iliyawezekudumukwamudamrefu, lakini pia kufikia maono na malengo haya basi ni lazima kuwe na utawala bora na tumeainisha mabadiliko ya kifikra na maridhiano katika kutekeleza majukumu haya”.

Washiriki wa kongamano hilo wametoka nchi mbalimbali ikiwemo Burundi, Ethiopia, South Afrika, Sudan, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan ya Kusini, Tanzania na  Uganda.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.