Monday, February 23, 2015
UTALII
NA, PETER FABIAN, MISUNGWI.
NAIBU Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia Madini, Charles Kitwanga, amewataka wachimbaji wadogo wa
Madini kujiunga katika vikundi ili kupatiwa Leseni za uchimbaji na mkopo wa fedha za ruzuku ya Sh bilioni 9 iliyotengwa na Serikali kwa wachimbaji wadogo ili kuwawezesha pia kupata vifaa vya uchimbaji.
Kitwanga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi
mkoani Mwanza alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wananchi wa vijiji
vya Mwagimagi na Mwamala akiwa katika ziara ya jimboni humo na kushiriki
uzinduzi wa nyumba mbili zilizojengwa na Mzawa mwekezaji wa Kampuni ya Mwamala
Gold Mine na kuzikabidhi kwa mzee Jadima Nkwabi katika kijiji cha Mwamala.
Naibu Waziri, Kitwanga alisema kuwa Serikali kupitia
Wizara ya Nishati na Madini imetenga Shilingi bilioni 9 ili kutoa ruzuku ya
mkopo kwa wachimbaji wadogo wa madini katika maeneo mbalimbali hapa nchini
kuliko na shughuli za wachimbaji ikiwa ni lengo la kuwasaidia mitaji ikiwa ni
kusaidia kukuza sekta hiyo ya Madini nchini.
“Tumelenga kuwasaidia wachimbasji wadogo hivyo ni
vyema mkajiunga katika vikundi na kuomba Leseni za uchimbaji itakayowasaidia
pia kupata mikopo ya fedha za ruzuku zilizotengwa na Wizara kwa wachimbaji
wadogo badala ya kung’ania kuchimba kila mtu,”alisema.
Kitwanga alisema wachimbaji mkiungana katika vikundi
na kupewa Leseni, Wizara itawapatia wataalamu wa kuwasaidia kuwaonyesha sehemu
zenye Madini kwenye maeneo yenu ambapo inaonyesha madini kutokuwa mbali sana ili
kuwawezesha pia kupata vifaa vya uchimbaji kwa mkopo mkiwa katika vikundi vyenu
ili kuwalahisishia kufanya shughuli zenu.
“Wizara tayari imeisha toa Leseni 27 kwa wachimbaji
wadogo katika maeneo ya vijiji vya Mwamazengo (7), Ishokela (7), Mwagimagi (2)
na Nyang’omango (11) Wilayani hapa katika maeneo yalipatikana Madini ambapo
wachimbaji wanatakiwa kuchimba kwa kufuata sheria ya Madini ya mwaka 2010,”alisisitiza.
Awali Mwekeaji wa eneo la kijiji cha Mwamala, Mkurugenzi
wa Kampuni ya Mwamala Gold Mine, Sultan Mohamed, anayetaraji kuanza uchimbaji
kijijini hapo alimwelea Naibu Waziri Kitwanga, akiwa mzawa na kuomba na
kupokelewa kuwa mwanakijiji kwa kununua shamba ambapo sasa ameamua kujikita
kuwa mchimbaji wa eneo hilo amechangia maendeleo katika kijiji hicho.
“Kabla sijachimba nimejenga nyumba mbili za thamani
ya Sh 15 na kumkabidhi mzee Nkwabi ambaye aliniuzia shamba lake ikiwa ni
kumuwezesha pia kuishi katika makazi bora pia nimetoa vifaa vya ofisi ya kijiji
cha Mwamala amapo nimetoa Komputa (1) na Printe yake, Kabati la kuhidhadhi
mafaili (1), Mihuri ya kisasa ya Ofisi (2), Saa ya Ukutani (1), Viti 30 vya
Plastiki na kutoa Mkufunzi mmoja wa Komputa,”alisema.
Mohamed alisema kwamba kutokana na kubaliwa kuwa
mwekezaji na wanakijiji hicho atafuata taratibu zote za ushirikishwaji wa jamii
na kuhifadhi mazingira atakapoanza ualishaji kutoa kipaumbele cha ajira kwa
vijana wa kijiji hicho kwa kufuata Sera, taratibu na sheria za Kampuni wa uchimbaji
endelevu wa kisasa wa kutumia Teknolojia na kuachana na uchimbaji duni.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.