TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wateja watatu Dar wakabidhiwa magari na Airtel baada ya kuibuka washindi Dar es Salaam, Februari 24, 2015 MWANAMKE mchuuzi wa mboga mboga katika Soko jipya la Kawe jijini Dar es Salaam, Grace Pascal Kalengera, jana alikuwa miongoni mwa wakazi watatu wa Dar es Salaam waliokabidhiwa zawadi zao baada ya kushinda promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi.
Ijumaa iliyopita, Grace alipigiwa simu na Balozi wa Airtel Yatosha Zaidi, mwigizaji maarufu nchini, Lulu, baada ya namba yake kuwa miongoni mwa washindi kwenye droo iliyochezeshwa makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kuigiza nchini. Siku nne tu baadaye, leo Jumanne, Meneja Masoko wa Airtel, Frederick Mwakitwange, alimkabidhi gari lake mama huyo aliyeonekana wazi akiwa na furaha isiyo kifani.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mwakitwange alisema: “Sisi Airtel, tunafarijika sana tunapowaona washindi wakimiminika ofisini kwetu kila wiki kujichukulia zawadi zao. Na kwa ukweli zawadi ya gari si zawadi ndogo kwa wengi miongoni mwetu.
“Tuliamua kwa makusudi kabisa kutoa magari kama zawadi kwa washindi kwa lengo la kuonyesha nia yetu ya kuboresha na kuyabadili maisha ya Watanzania.” Mbali na Grace, washindi wengine waliokabidhiwa magari yao ni pamoja na John Freddy Kiwale mkazi wa Kinondoni ambaye pia ni wakala wa Airtel Money na Donald Fred Baruti mfanyabiashara wa Mwembechai Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando, alitoa wito kwa wateja wa kampuni hiyo kuendelea kutumia huduma za Airtel Yatosha Zaidi waweze kupata nafasi ya kujishindia magari.
“Kama mnavyoona, hata mawakala wa Airtel Money wanaweza kushinda. Hii ni kwa sababu tu kwamba nao pia ni wateja wetu. Inafahamika kuwa kuna vigezo na masharti katika kushiriki na sisi tunazingatia sana hilo,” alisema Mmbando.
Washindi wengine wa wiki iliyopita watakaopewa magari ya oleo ni Simon Grayson (Yombo, Kisiwani), Bilal Juma Mlendela (Tabata) na Maxbeth Isack Manene (Tabata Segerea), kisha mkazi na mkulima kutoka Bukoba, Kajala Kokutima Said, naye atapewa gari wiki hii. Tayari magari 17 kati ya 60 yamekwishapata wamiliki wake wapya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.