ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 12, 2015

FEBRUARI 20 NDIYO MWISHO WA KUPOKEA FOMU ZA SAFARI WEZESHWA MSIMU WA 4.

 SAFARI LAGER WEZESHWA MSIMU WA IV YATANGAZWA MWISHO WA KUJESHA FOMU.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dar es Salaam, Alhamisi 12 Februari, 2015: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza tarehe ya mwisho ya kurejesha  fomu za programu yake ya Safari  Lager Wezeshwa kwa msimu wa nne kwa wajasiriamali wadogo wadogo  na wa kati  Nchini.  

Akizungumza  na waandishi wa habari, Meneja wa bia ya Safari Lager Bi. Edith Bebwa  alisema, “ Ijumaa tarehe 20 Februari ni siku ya mwisho ya kurudisha fomu za wanaotaka kujiunga na programu ya Safari Lager Wezeshwa .

Alisema Edith tunawakumbusha wale mliochukua fomu na hamjarudisha basi mtumie muda huu kuziresha fomu mahala mlipochukulia na kwa wale ambao hamjachukua bado tuna muda wa takribani siku saba  za kuchukua fomu kujaza na kuiresha ulipochukulia.

  Fomu za ushiriki zitapatikana kwenye mabohari ya TBL, Mawakalai wa kusambaza bia za TBL, kwenye mtandao wa www.wezeshwa.co.tz . Fomu hizo zichukuliwe, zijazwe na kurejeshwa kwenye vituo vilivyotajwa hapo juu au kwa njia ya posta kwa sanduku la posta (Safari Lager Wezeshwa msimu wa nne,TBL Dar es Salaam,P.O Box  9013 DSM), kabla ya tarehe 20 Februari 2015.

Programu hii inafanyika takribani mikoa yote ambapo itawapa fursa wajasiriamali wa aina zote bila kujali fani,kabila wala jinsia  kujaza fomu kwa usahihi na kamilifu kisha kuzirudisha mahala husika na baadae waliokidhi nafasi zinazohitajika kuchaguliwa kisha kupewa mafunzo mafupi  pamoja na kukabidhiwa ruzuku zao.


Nae kiongozi wa wataalamu wa ushauri wa biashara kutoka kampuni ya TAPBDS, Bwana Joseph Migunda alisema kuwa  “Zoezi hili linahusisha wataalamu wenye uwezo na uzoefu mkubwa katika kushauri na kusaidia ukuzaji wa sekta ya biashara ndogo na kubwa. Hivyo aliomba wajasiriamali wote kuitumia fursa hii kushiriki kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa kwenye fomu ya ushiriki. Wenye nia ya kufika mbali kibiashara na wenye  malengo ya kuisaidia jamii inayowazunguka wasisite kuchangamkia fursa hii”.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.