Rais wa Ivory Coast Alassane Quattara (kushoto akipiga makofi) wakati wa mapokezi ya mabingwa wa Africa Ivory Coast, pia anaonekana nahodha wa timu hiyo Yaya Toure. |
RAIS wa Ivory Coast Alassane Ouattara ametoa zaidi ya €3 milioni ($3.4m) kama bonasi kuwatuza washindi wa Kombe la Taifa Bingwa Afrika 2015, Wizara ya Michezo nchini humo ilisema Jumanne.
Taifa hilo la Afrika Magharibi lililaza Ghana 9-8 kupitia mikwaju ya penalty baada ya kutoka sare tasa muda wa kawaida na wa ziada Equatorial Guinea na kuinua taji lao la pili, la mwisho likiwa 1992.
Kocha Herve Renard alialikwa ikulu ya rais Jumanne huku Mfaransa huyo akipokezwa bonasi ya takriban €114 000 ($129.000).
Wachezaji wake 23 walipokezwa nyumba za thamani ya €46 000 ($52 000) kila mmoja pamoja na pesa taslimu kiasi sawa, kwa mujibu wa Waziri wa Michezo Alain Lobognon.
Shirikisho la Soka la Ivory Coast €380 000 ($429 000), huku wakufunzi na wafanyakazi wengine wakigawana €460 000 ($520 000), pesa hizo zote kwa jumla zikiwa €3milioni.
Kikosi chote pia kitapewa tuzo ya cheo cha hadhi ya walinzi wa kitaifa kwa kiingereza Knights of the National Order.
"Asanteni sana, Ivory Coast sasa imeungana tena,” akasema Ouattara, akiongea kwa kina kuhusu umoja ambao umeletwa na ushindi huo.
"Mlifanikiwa kuunda tena timu imara na kutia bidii kufikia lengo moja – kushinda na kushinda zaidi. Ni funzo kwetu katika kuleta pamoja watu,” akasema.
Ndovu hao wa Ivory Coastw ameonekana kama nguvu ya kuleta pamoja taifa lao ambalo ni moja ya mataifa maskini zaidi duniani, na linajikwamua kutoka kwa miaka 10 ya mtafaruku wa kisiasa na mzozo wa kivita.
"Tumekuwa tukiota kuhusu taji hilo kwa robo karne! Sasa kikombe kiko hapa, na kama wasemavyo mambo mema huja yakiwa matatu matatu!,” alasema Ouattara. CHANZO: SuperSport
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.