ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 14, 2015

TOTO YAIBAMIZA POLISI TBR 2-1

Wachezaji wa timu ya Polisi Dodoma wakimchimba mikwara na kumnyooshea kidole Mwamuzi Line One Jamada Amada.
Mwamuzi Line One Jamada Amada akienda chini mara baada ya kupigwa makonde ikiwa ni sanjari na kuzabuliwa vibao.
'Hapa ngwala, ngumi na vibao'  Toka kwa wachezaji wa Polisi Tabora wakimzonga na kumshambulia mwamuzi Line One Jamada Amada wa mchezo wao dhidi ya Toto Africans uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wachezaji wa Polisi Tabora wakimzonga na kumshambulia mwamuzi Line One Jamada Amada wa mchezo wao dhidi ya Toto Africans uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

NA. ALBERT GSENGO:MWANZA

TOTO Africans ya jijini Mwanza hii leo imefanikiwa kugeuza matokeo katika dakika za mwishoni mwa mchezo dhidi ya Polisi Tabora ambayo ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 hadi dakika ya 86 ya mchezo mfungaji akiwa Hamisi Twaha aliyeifungia Polisi goli hilo kwa njia ya penati.

Hata hivyo mchezo wa leo ulikuwa kama hadithi vurugu za hivi majuzi iliyojirudia tena kwani mchezo wa leo nao ulilazimishwa kumalizika kwa style ya wachezaji kumpa kichapo mwamuzi Line one wa mchezo huo Jamada Amada, wakidai amewauma kwani walikuwa wamepaki basi huku wakicheza offside trick.

Amada alilazimika kujisalimisha kwa kutimua mbio hadi vyumbani jukwaa kuu. 

Toto Africans ilisawazisha kupitia mshambuliaji wake James Magafu, huku bao la ushindi likifungwa na Jafari Mohamed. (BOFYA PLAY KUSIKILIZA SAUTI RIPOTI YA SPORTS XTRA)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.