ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 14, 2015

MHUDUMU AMFIKISHA MAHAKAMANI MBUNGE MACHEMLI KWA MADAI YA KUSHINDWA KUMLIPA MSHAHARA WA MIAKA MITATU.

Machemuli bungeni.
NA MWAANDISHI WA BLOG HII, MWANZA. 

MBUNGE wa Jimbo la Ukerewe, Salvatory Machemuli (Chadema), amefikishwa katika Mahakama ya Kazi akidaiwa mshahara wa miaka mitatu na mhudumu wa Ofisi yake ya Mbunge wa Jimbo la Ukerewe jijini Mwanza. 

Machemuli amefunguliwa shauri la madai katika mahakama hiyo na kupewa nakala ya kuitwa yenye Na MCA/MZ/UK/524/2014 katika mahakama hiyo baada ya kufunguliwa kesi na Rehema Hamis (Mhudumu) kwa madai ya kutomlipa mshahara wake kwa miezi 35 ikiwa ni kiasi cha Sh milioni 3,680,000 alizotakiwa kulipwa.

Madai yaliyofunguliwa na Rehema ni pamoja na mapunjo ya mshahara kwa miezi 35, malipo ya likizo ya miaka mitatu, kusimamishwa kazi bila kulipwa haki sitahiki na posho ya likizo ambapo jumla yake ikiwa kiasi cha milioni 3,680,000/= ambazo amefunguliwa madai.

Akizungumza na GSENGO BLOG hii leo nje ya jengo la Ofisi za Idara ya Kazi jijini Mwanza kulipo na Mahakama hiyo Wakili wa Kujitegemea anayemtetea Mbunge Machemuli, Mathew Nkanda alisema kuwa shauri hilo limeailishwa kutokana na Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mussa Katamulo, kuwa nje ya Mkoa wa Mwanza kikazi.

Wakili Nkanda alisema kuwa pamoja na mteja wake kutoonekana mahakamani hapo kutokana na kuwa na majukumu mengine ya uwakilishi huko jimboni Ukerewe pia kuhudhulia Kesi nyingine leo hakukuweza kuwasili mahakama kuisikiliza na badala yake imepangwa kusikilizwa tena Januari 28 mwaka huu.

Mbunge huyo amekuwa akikabiliwa na Kesi zaidi ya tatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mfawidhi Wilaya ya Ukerewe jambo lililobainika kushindwa kufika jijini Mwanza leo kuhudhulia shauri hilo ambapo taarifa kutoka Wilayani Ukerewe zimedai kuwa alikuwa huku ambapo leo alikuwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Mjini Nansio kuhudhulia katika kesi nyingine.

Naye mlalamikaji Rehema alisema kuwa amekuwa akimdai mbunge huyo bila mafanikio na badala yake kukabidhiwa barua ya kuachishwa kazi kufuatia kumdai, ambapo pia alikiri kulipwa na Machemli kwa miezi minane kiasi cha shilingi elfu 50 kila mwezi kinyume na sheria na kanuni za kima cha chini cha mshahara ulio tangazwa na Serikali.

Machemuli kesho  Alhamisi atahudhulia Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ukerewe kusikiliza hukumu ya kesi aliyofunguliwa na mfanyabiashara wa Mjini Nansio, Paschali Munubi, kesi Na 1/2014 ya Madai ya kununua nyumba iliyouzwa kwa amri ya Mahakama na Dalali wa Mahakama hiyo, Kampuni ya Eldang Auctioneer ya jijini Mwanza.

Machemuli alifunguliwa shauri hilo la madai na mfanyabiashara Mnubi kutokana na kuvunja makufuri na kuingia kwa nguvu ndani ya jengo la Munubi Nyumba ya Kulala wageni na Bar na kujichukulia mali ya ndani ikiwa ni TV zaidi ya 10, Magodoro, Friji zaidi ya tatu, Vinywaji ikiwa ni soda, bia na pombe kali bila Hati ya Ununuzi kutoka Mahakama iliyoamuru kuuzwa jengo hilo.

Habari zaidi zilizopatikana kutoka Wilayani humo zimeeleza kuwa kutokana na hatua hiyo ya kuingia kwa nguvu pamoja na kununua jengo hilo kwa kiasi cha Sh milioni 28 tasilimu na baada ya mmiliki wake kumtaka Mbunge amruhusu kuchukua mali na vifaa vyake hivyo na kukataa wakati akiwa amenunua jengo tu na si mali na vitu ningine vya biashara vilivyokuwemo ndani ya jengo hilo.

“Mfanyabiashara huyu alidai kwa kumfikisha katika Ofisi ya Mwenyekiti wa Kitongoji bila mafanikio, akaenda Ofisi ya Mtendaji na Mbunge aligoma na kisha Mnubi kwenda kwa Ofisi ya Mwanzasheria na kupewa hati ya siku saba kumkabidhi mali yake lakini alikaidi hati hiyo ya mwaka 2012 hadi alipofunguliwa kesi ya madai mwaka jana, ambapo kesi hiyo pia amekuwa hahudhulii,” alieleza mmoja wa ndugu zake Mbunge ambaye hakutaka jina kuandikwa gazetini.

Mbunge Machemuli katika kesi hiyo kesho anatarajiwa kutolewa uamuzi na Hakimu Kisheni aliyekuwa anaisikiliza kesi hiyo baada ya kukamilika kwa ushahidi wa pande zote zilizotakiwa kutoa ushahidi mahakamani hapo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.