ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 13, 2015

SIMBA BINGWA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI 2015

Fainali ya Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015 imefanyika usiku huu katika uwanja wa Aman mjini Zanzibar, ambapo Simba Sports Club walikuwa wakipepetana na Mtibwa Sugar.

Mbele ya mgeni rasmi Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr. Mohamed Shein, Simba wameibuka washindi na kutwaa U-champion kwa kuifunga Mtibwa Sugar kwa mikwaju ya penati 4 - 3.

UPIGAJI WA PENATI:- 
Simba:- Awadh Jumaa 1
Mtibwa:- Ally Lundenga 1
Simba:- Shahban Kisiga 0 Kipa Said Mohamed kacheza
Mtibwa:- Shahban Nditi 1
Simba:- Kessy Ramadhan 1
Mtibwa:- Ibrahim Jeba 0 Ikagonga mwamba.
Simba:- Isihaka Hassan 1
Mtibwa:- Ramadhan Kichuya 1
Simba:- Danny Serunkumah 1
Mtibwa:- Vicent Barnabas 0 Kipa Ivo Mapunda aicheza penati.

ZAWADI NYINGINEZO:-
Kipa bora ni Said Mohamed wa Mtibwa Sugar.
Mchezaji bora wa Michuano ni Salim Mbonde wa Mtibwa Sugar.
Mfungaji bora wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi ni Simon Msuva wa Yanga Africans.

Mabingwa Simba wamepata zawadi ya kitita cha shilingi milioni 10, ile hali Mtibwa wameambulia shilingi milioni 5.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.