ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 18, 2015

MFANYABIASHARA NA MTUHUMIWA SUGU WA UJAMBAZI ANASWA NA SMG NA RISASI 331, MAGAZINE 9 NA MIFUPA MI3 INAYODHANIWA KUWA NI YA BINADAMU

Wakizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Mwanza, Makamanda wa Polisi SCP Valentino Mlowola wa mkoa wa Mwanza (katikati) SCP Charles Mkumbo wa mkoa wa Shinyanga (kushoto) na  SCP Justus Kamugisha wa mkoa wa Simiyu(kulia).
JESHI la Polisi limefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa sugu ambaye pia ni kiongozi wa ujambazi mfanyabiashara aitwaye Njile Samweli (46) marufu kwa “John” wa mijini Bariadi mkoani Simiyu kwa tuhuma za ujambazi ambaye ni Kiongozi Mkuu wa mtandao ya Ujambazi, aliyekuwa akifanya matukio ya uhalifu katika Mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Singida na Tabora.

Mtuhumiwa huyo aliyekuwa pia akiwauwa washirika wake mara baada ya kufanya matukio ya uhalifu katika Mikoa hiyo amekamatwa na kikosi kazi cha ushirikiano cha Jeshi la Polisi kutoka Mikoa hiyo kilichokuwa kikimsaka kwa muda mrefu.

Wakizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Mwanza, Makamanda wa Polisi SCP Valentino Mlowola (Mwanza),SCP Charles Mkumbo (Shinyanga) na  SCP Justus Kamugisha (Simiyu), Kamanda Mlowola alisema kuwa mtuhumiwa huyo mfanyabiashara wa mjini Bariadi mkazi wa kijiji cha Lyoma alikamatwa  Januari 5 mwaka huu wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu.

Kamanda Mlowola alieleza kuwa kukamatwa kwa kiongozi huyo hatari wa kundi la ujambazi katika mikoa hiyo kumetokana na kukamatwa mmoja wa washirika wa kundi lake Januari 5 jijini Mwanza kutokana na taarifa za siri kutoka kwa rai wema waliotoa kwai Polisi na Jeshi la Polisi Mkoa kuunda kikosi kazi kushirikisha mikoa hiyo cha kufatilia mtandao huo na kufanikiwa kuwakamata.

Aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Mabula Lyanga (36) maarufu kwa jina la Magana mkazi wa kijiji cha Bugarama wilayani Maswa Mkoa wa Simiyu akiwa na jeraha la kupigwa risasi na jambazi mwenzake aitwaye Njele (Kiongozi wa kundi) kwenye bega lake la kulia kutokana na raia wema kumtilia mashaka na kuanza kumfatilia na kunaswa na polisi.

“Baada ya kumkamata mtuhumiwa huyu wa ujambazi katika mahojiano na askari wetu alimtaja mtuhumiwa mwenzake Njile kupiga risasi wakiwa katika harakati za tukio la ujambazi wa kutumia silaha katika kijiji cha Idukilo Kata ya Luhumbo Mwadui wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga Januari 5 mwaka huu,”alieleza.

Kamanda Mlowola alisema kuwa watuhumiwa hawa baada ya kufanya uhalifu huo na uporaji na kutofautiana na kiongozi wake Njile limfyatulia risasi mbili na kumjeruhi kweny bega, tuliwatuma askari wa Idara ya Upelelezi kutoka Mwanza kwenda kufatilia na kufanya msako mkali kwa kushirikiana na wenzao wa Bariadi mkoani Simiyu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu, Justus Kamugisha akiwasilisha taarifa kwa waandishi wa habari.
“ Kikosi kazi chetu kilifanikiwa kumkamata Njile na katika mahojiano naye binafisi alikiri kuhusika na tukio hilo na kuelezea kufanya matukio mengine mengi katika Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora ikiwemo kuwauwa washirika wenzake na kuwataja wengine ikiwemo alipokuwa amehifadhi silaha (SMG) risasi 331 na Magazine tisa vilivyotumika,”alisema.
SCP Mlowola alitaja matukio kadha waliyofanya watuhumiwa hao katika Mkoa wa Mwanza kuwa ni pamoja na kuvamia na kupora fedha kiasi cha Sh milioni 3,500,000/= katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Samba katika Kisiwa cha Bulubi wilayani Ukerewe Agosti mwaka 2014, Oktoba 2 mwaka 2014 katika Kijiji cha Mahaha walivamia maduka kadhaa na kupora fedha kiasi cha Sh milioni 3 na Pikipiki moja na kumuua mtu mmoja.

Tukio jingine lilifanyika Oktoba 2014 eneo la Malya wilayani Ngudu ambapo walivamia na kupora fedha kiasi cha Sh milioni 2 na kumjeruhi mtu mmoja na wahusika wa matukio yote hayo walioshiriki ni Njile (kiongozi), Lyagwa (aliyepigwa risasi na Njile), Magingi Doto “Kafuru”,Thomas, Daniel Pastory, Mashauri Ngulyati, Kipisto Chenya.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoawa Shinyanga SCP Charles Mkumbo akionesha silaha iliyokuwa ikitumiwa katika harakati za matukio ya ujambazi katika kijiji cha Idukilo Kata ya Luhumbo Mwadui wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoawa Shinyanga SCP Charles Mkumbo akionesha nyguo ambazo zilikutwa kwa kiongozi huyo wa genge la uhalifu ambazo zinasemekana ni za baadhi ya watu waliouawa wakiwemo majambazi aliokuwa akishirikiana nao ambao aliwauwa kwa maslahi yake.
"Hii ni mifupa tuliyoikuta nyumbani kwa mtuhumiwa"
Naye Kamanda SCP Mkumbo ( Simiyu), alisema kwamba baada ya kikosi kazi kufanya ufatiliaji kutokana na maelezo ya mtuhumiwa Njile walifanikiwa kukamata bunduki moja ya kivita (SMG )yenye namba BP 3402, risasi 331, Magazine tisa, mifupa na nguo zinazosadikiwa kuwa  ya marehemu waliouwawa mtuhumiwa huyo.

Alisema mtuhumiwa huyo na washirika wake waliafanyua matukio mengine ya uhalifu katika wilaya ya Itilima ,Maswa, Meatu ,Bariadi ambapo walipora Sh.20.5 milioni.

Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga, SCP Kamugisha,alisema watuhumiwa hao walifanya uhalifu katika wilaya ya Kishapu walikopora Sh.3.2 na simu aina ya Nokia pia walimjeruhi mwenzao (Mabula Lyagwa) kwa risasi kabla ya kumbeba na kumtelekeza mjini Maswa.

Alisema walifanya matukio mengine katika wilaya ya Igunga,kwa kupora simu na fedha,pia walipora mkoani Singida kiasai cha Sh.1.5 na hadi sasa jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa watano na wengine bado wanatafutwa, mara baada ya taratibu kukamilika watafikishwa mahakamani.
Wanahabari tukioni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.