ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 13, 2015

JEH MARA QUEENS WATALIPIZA KISASI HII LEO?


NA WILSON ELISHA:-

TIMU ya soka ya wanawake ya Mkoa wa Mara, Mara Queens hatimaye imemaliza kuweka kambi yake kwa ajili ya kulipiza kisasa katika mchezo wa marudiano na Mwanza Queens, kufuatia kipigo cha mabao sita kwa moja walichokumbana nacho kwenye ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Taifa la wanawake (Taifa Cup) mchezo uliofanyika jijini Mwanza. 


Timu hiyo ya wanawake ya Mkoa wa Mara iliweka kambi jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kulipa kisasi ili iweze kusonga mbele katika mashindano hayo.

 Wachezaji wa timu ya soka ya wanawake  ya Mkoa wa Mara, Mara Queens  wakijifua kwa mara ya mwisho katika kambi yao waliyoiweka jijini  Mwanza kwa ajili ya kujiandaa na  mchezo wa marudiano  baina ya timu ya soka ya wanawake ya  Mkoa wa Mwanza  Mwanza Queens unatakaofanyika leo mkoani Mara.
 Nyoosha mwili na mazoezi ya viungo.
Gsengo blogu imeshuhudia  wachezaji hao  wakifanya mazoezi na kuelezea matumani yao katika mchezo wa marudiano Mkoani Mara huku wakilalamikia uongozi wa Mkoa wa Mara kwa kushindwa kuwasaidia vifaa vya michezo.
Mara Queens.
Katibu wa Mara Queens  Sure Mugeta  amesema  wameweka kambi  jijini  Mwanza kutokana na kudhaminiwana  na  mdau wa michezo ambaye ni m kurugenzi wa kituo cha michezo cha Alliance James Bwire na kutoa wito kwa wadau wengine wa Mkao  wa Mara kuiga mfano  huo kwa kutoa msaada wa hali na mali ili waweze kufanya vizuri zaidi.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Msakato Magai (kulia mwenye jezi namba 3) amesema anauhakika wakufanya vizuri katika mchezo wa marudiano kutokana na mazoezi ambayio wameyafanya na wachezaji wake wote wako vizuri. 

Katika mchezo wa  kwanza wa ufunguzi  wa kuwania kombe la Taifa la wanwake  baina ya Mara Queens  na Mwanza Queens  timu hiyo ilichpwa mabao sita kwa moja  na  mchezo wa  marudiano baina ya timu hizo unapigwa  katika uwanja wa Karume mjini Musoma  January 13 mwaka huu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.