ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 29, 2014

WASHINDI WA DROO YA TATU YA COCA COLA WAJINYAKULIA ZAWADI AKIWEMO MSHINDI WA TV FRAT AINA YA SONY JIJINI MWANZA LEO

Mkuu wa Idara ya Mauzo wa Kampuni ya Nyanza Bottiling Ltd (NBCL) Japhet Kisusi (wapili kutoka kulia), akimkabidhi mshindi wa TV Frat aina ya Sony, Paul Alex wa Bariad Bar, huku Maafisa mauzo wa NBCL, kutoka kushoto ni Pramod Sahu, Pramod Nair na kulia ni Albert Nswanzugwako katika droo ya tatu iliyofanyika leo katika ukumbi wa Makutano Mwanza Hoteli.
Afisa Mauzo wa Nyanza Bottiling Tld (NBCL) Pramod Nair akisubili kupokea tiketi ya mshindi kutoka kwa mmoja ya wateja aliyepewa nafasi ya kuchukua ndani ya box la kuchezeshea droo ya tatu.
Mmoja wa washindi wa Kreti 10 kila mmoja kati ya 20 walioshinda katika droo ya tatu akikabidhiwa zawadi yake na Afisa mauzo wa eneo analotoka leo katika ukumbi wa Makutano Mwanza Hoteli.
Magret Gelard wa Home Park Bar akitoa tiketi ya kumtangaza mshindi wakati wa droo iliyofanyika leo.
Mmoja wa washindi akifurahia kuibuka na ushindi wa Kreti 10 za soda za Coca Cola akiwa na Afisa mauzo wa eneo lake leo katika droo ya tatu ya NBCL jijini Mwanza.
Nimeshinda angalieni tiketi yangu huyu ni mshindi wa Kreti 10 za soda za Coca Cola akiwaonyesha Maafisa mauzo wa NBCL.
Mkuu wa Idara ya Mauzo wa Kampuni ya Nyanza Bottiling Ltd (NBCL) Japhet Kisusi akishuhudia tiketi ya mshindi aliyetangazwa na mmoja ya wateja walioshiriki kuchezesha droo ya tatu leo jijini Mwanza.
Mkuu wa Idara ya Mauzo ya NBCL Japhet Kisus akimkabidhi cheti cha shukurani mmoja ya wateja waliofanya vizuri katika kununua na kupanga vyema soda za Coca Cola katika Freji
Afisa mauzo wa NBCL akikabidhi zawadi ya saa ya ukutani kwa mshindi wa droo ya tatu iliyofanyika leo
Hongera kwa ushindi wa zawadi ya saa ya ukutani.
Maandalizi kabla ya kuanza kwa droo ya tatu kupata washindi leo
Mkuu wa Idara ya Mauzo ya NBCL Japhet Kisus akimkabidhi mteja Bitrice Denis kutoka Hoteli ya MS ya kona ya Bwiru zawadi ya Sh 50,000/= tasilimu baada ya kuibuka mshindi wa papo kwa papo katika droo iliyofanyika leo.
Wakati wa kupata chakula.
Maafisa mauzo wa NBCL na Wanahabari wakichukua chakula.
Mwalimu wa Mafunzo ya Biashara wa bidhaa za Coca Cola (NBCL) Japhet Kubebeka akifafanua jambo kwa wateja walioshiriki droo ya tatu ya shindano la "Coke Display Competion" wakati wa chakula cha pamoja baada droo hiyo lililofanyka leo ukumbi wa Makutano Mwanza Hoteli.
Tujipogeze kwa chakula cha pamoja
Mkuu wa Idara ya Mauzo wa NBCL, Japhet Kisusi akizungumza na wanahabari leo ikiwa ni pamoja na kujibu maswali yao.
Picha ya Maafisa wa Idara ya Mauzo ya NBCL na Washindi wa droo ya tatu ambao wamepata zawadi za soda, saa za ukutani, vuvuzera,mipira ya miguu na TV Frati kwa Mshindi wa kwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.