UTEJA WA DAWA ZA KULEVYA UNACHANGIWA
NA UNYANYAPAA TOKA KWA JAMII
Na: Edwin
soko
Mwanza
Tabia ya
jamii kuwanyanyapaa watumiaji wa dawa za kulevya imekuwa ikichangia kwa kiasi
kikubwa wateja wa dawa
za kulevya waliacha kurejea
matumizi ya dawa
hizo na matokeo kuthidi
kuathirika kimatendo kiroho na kimwili.
Makala hii
ilijikita kutazama mtazamo wa
jamii juu ya waliokuwa
wateja wa dawa za kulevya
baada ya kupata
program maalumu toka
kwenye Nyumba za utimamu (Sober Houses) na
wanaopata tiba ya methadone
toka kwenye kiliniki za Muhimbili, Mwanayamala na
Temeke.
Ni imani yangu
kuwa, tiba hizo
mbili ni msaada mkubwa kwa
wateja wa
dawa za kulevya, endapo
mtu atajitambua na kujikubali
ni wazi kuwa ataachana
na maisha ya uteja
wa dawa za kulevya na kuishi
maisha huru bila kuwa
mtumwa wa dawa za kulevya.
Jamii ina wajibu mkubwa kwa waliokuwa wateja wa dawa
za kulevya katika kuhakikisha kuwa hawanyanyapaliwi ili
wasiweze kurudi tena kwenye
matumizi ya dawa za kulevya kwa kupata
upendo mkubwa toka kwa familia, ndugu na marafiki. Suala hili
limekuwa gumu sana
kwa jamii, kwani watu wengi wamekuwa
hawana imani tena
kwa mtu aliyekuwa akitumia dawa
za kulevya na baadaye
kuamua kuacha.
Bwana Novatus William
mtumiaji wa dawa za kulevya anayepata
tiba ya utimamu wa mwili ya
Pili Missanah Mwamza alisema kuwa
mazingira ya awali
yana nafasi kubwa sana ya
kumrudisha mtu aliyekuwa mteja wa dawa za kurejea tena
kwenye matumizi ya dawa za
kulevya kwa kuwa jamii
inayomzunguka ina baki
na picha ile ile
ya uhalifu kwa mtu yule
yule. .
Naye Bwana Nicholus Manota toka
Nyumba ya utimamu
ya pili Missah alisema kuwa
familia za watu
waliokuwa wakitumia dawa za kulevya zinakosa kurudisha imani kwa
ndugu zao wanapoacha kutumia
dawa za kulevya baada
ya kutoka kwenye
nyumba za utimamu na
hali hiyo inapelekea
walioacha dawa kukosa
imani ya kuheshimiwa na jamii zao
na hali hizo zinapelekea
mtu kurudi katika
matumizi ya dawa kwa
lengo la
kupata faraja.
Pia Manota aliongeza kuwa,
hata jamii inayozunguka
nyumba za utimamu (Sober Houses) imekuwa haina
imani kabisa kwa kudhani
wao ni wahalifu wakati ilibidi
watambue kuwa wao ni watu
wenye matatizo ya kiafya
kama walivyo wagonjwa wengine na sio
wahalifu.
Naye meneja wa
nyumba ya
utimamu ya Pili Misanah kata
ya Ilongazala , wilaya ya Ilemela
Jijini Mwanza Bwana Mohammed Mohammed alibainisha
kuwa, tatizo kubwa
la wateja wengi walioacha
dawa za kulevya kurejea kwenye matumizi
ya dawa za kulevya ni
kukosekana kwa ushirikiano
toka kwa jamii, kwani
jamii imekuwa haitaki
kuamini kwamba mtu
anayetumia dawa za kulevya anaweza kupona na kurejea
katika hali yake
ya kawaida. Kitendo hicho
kimekuwa kikiwabagua wateja walioacha dawa za kulevya na
hatimaye kujikuta wametengwa na
jamii nzima na hapo
ndipo urudi kwenye kwenye
matumizi ya dawa za kulevya ili
kupata faraja.
Athari za matumizi ya dawa za kulevya zinaweza kuwa, kimwili, roho na akili |
Nyandidi aliongeza
kuwa wateja wa dawa za kulevya upendo
wa kijamii ili waweze
kuimarika kimwili na
kiroho na kujiona ni sehemu ya
jamii licha ya maovu
waliyokuwa wakiyafanya.
Naye Bibi
Rehema Abdallah aliyeacha
dawa za kulevya kwa kuhudhuria Kiliniki
ya Methadone ya Muhimbili
alimwambia mwandishi wa
makala hii kuwa, dawa za kulevya zinauwezo wa kuachwa
cha msingi ni
elimu kwa jamii
juu ya ukweli
huu, kwani jamii bado inamchukulia mteja wa dawa za kulevya sawa na
muhalifu.
Bwana Leonard
Cyprian mkazi wa Mabatini ,Wilaya
ya Ilemela Jijini
Mwanza alisema kuwa
jamii inaishi na ndoto
za vitendo viovu
vilivyokuwa vinafanywa na
wateja wa dawa za kulevya
hasa za
wizi na unyang’anyi
hivyo inakuwa vigumu
sana kwa mara
moja kuamini kuwa
mtu aliyekuwa mwizi
anaweza kuwa mwema.
Ni wazi kuwa
jamii inabidi ibadilike na kuamini kuwa mtumiaji wa
dawa za kulevya anaweza kupona
na kurejea katika maisha yake
ya kawaida, cha msingi
jamii iwe na upendo
na wale wote
walioacha kutumia dawa za
kulevya, kwani kuzidi kuwanyanyapaa
ni kuzidi kukuza tatizo badala
ya kupunguza tatizo, iwachukulie watu
hao kama wagonjwa
wengine wa malaria au Virusi
vya Ukimwi/AIDS.
Kwa ushauri wasiliana na Mwandishi wa makala
hii kwa simu 0754551306
Makala hii
imedhaminiwa na Mfuko
wa Kuvisaidia Vyombo vya Habari
Tanzania(TMF)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.