ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 5, 2014

PICHA ZA AJALI YA MAOFISA WA BOT WALIOFARIKI JANA MWANZA.

MAOFISA wawili wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) waliokuwa wakisafirisha fedha kutoka Mwanza kuelekea Shinyanga, wamefariki dunia baada ya ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali.

Katika ajali hiyo pia askari wawili wa Kikosi Maalumcha Kutuliza Ghasia (FFU) walijeruhiwa wakati wa ajali hiyo.
Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa ni baada ya gari hilo lililokuwa likiongoza msafara wa magari ya BOT kupinduka baada ya kumgonga mwendasha pikipiki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 7:45 mchana katika barabara ya Mwanza - Shinyanga, eneo la Bohari, kata ya Butimba.
Askari katika eneo la tukio wakiweka utaratibu.
Gari lililopata ajali ni lenye namba za usajili SU 35296
Kikosi cha ulinzi kikazi eneo la tukio.
Kamanda Mlowola aliitaja pikipiki iliyosababisha ajali hiyo ni yenye namba za usajili T 792 CTG.

"Baada ya pikipiki kuingilia msafara huo, iligongwa na gari la ulinzi lililokuwa kwenye msafara huo aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili SU 3526 mali ya Benki Kuu"

Kabla ya ajali hiyo, dereva wa gari la ulinzi alijaribu kumkwepa mwendesha bodaboda, lakini kutokana na msafara huo kuwa na mwendo mkali, lilipasuka tairi la mbele na kukosa mwelekeo hivyo kupinduka.

"Pamoja na ajali hiyo, magari yaliyokuwa yamebeba fedha yapo salama, hakuna upotevu wowote wa fedha kwasababu askari waliokuwa kwenye magari mengine walichangamka na kuimarisha ulinzi wakishirikiana na askari wa JWTZ" alisema Kamanda Mlowola.
Kamanda aliwataja waliofariki katika ajali hiyo ni dereva wa gari lililopata ajali Mohamed Mumba na Beatrice Lumelezi ambaye ni Ofisa wa BOT.

" Majeruhi ni watatu ambao kati yao ni askari wawili pamoja na dereva wa bodaboda ambaye nimeelezwa kuwa ana hali mbaya. "Miili ya waliofariki imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando na majeruhi wamelazwa hospitalini hapo kwa matibabi zaidi" alisema
Kampuni maalum Mwanza ikifanya kazi kuliondoa gari la maofisa wa BOT waliopata ajali.
Hali halisi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.