KIKUNDI CHA
ELIUD PROSPER MABINGWA MBIO ZA BALIMI MITUMBWI KAGERA.
Na
Mwandishiwetu, Kagera.
KIKUNDI cha
Wanaume wapiga kasia cha
Eliud Propsper Mkoani Kagera kimeibuka na ubingwa katika fainali za Mkoa za mashindano ya mbio za mitumbwi chini ya udhamini wa bia ya Balimi
Extra Lager zijulikazo kama “Balimi Boat Race 2014”
na hivyo kikundi hicho kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 900,000/=
pamoja na kuwakilisha Mkoa wa Kagera kwenye fainali za Kanda
zinazotarajiwa kufanyika Desemba 6 mwaka huu jijini Mwanza.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi
cha Zadock
Ezekiel ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/=
pamoja na kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza pia,
wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha
Eliakim Zadock ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 500,000/=
na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Steven Nestor
ambacho kilizawadiwa Shilingi 400,000/=.
Nafasi ya tano hadi ya tisa walipewa kifuta jasho
cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi ambavyo ni Laurent Laurian, Alex
Andrew, DaliusKiiza, Edwin John, Mwesiga Dan na Johnson John.
Upande wa Wanawake kikundi
cha Khadija
Ramadhan kilifanikiwa kutwaa ubingwa na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 700,000/=
pamoja na nafasi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda
jijini Mwanza.
Nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na kikundi cha Salome Elnest ambao walizawadiwa Shilingi 600,000/=, washindi wa tatu ni kikundi cha Fredina Enerico ambao walizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Agnes Matunga ambao walizawadiwa Shilingi 300,000/= na nafasi ya tano hadi ya kumi walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi 200,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Halima Ahmad, Melesiana France, Anagrace Joseph, Paxdia Baituna Zuhura Abdala.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi Meneja Matukio wa
Kanda ya Ziwa TBL, Erick jitokeza kushiriki fainali hizo na kuwaomba waendelee na maandalizi vyema kwa fainali za
Kanda zinazo tarajiwa kufanyika Desemba 6, mwaka huu jijini Mwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.