Airtel yazindua huduma mpya kwa wateja wake kupata huduma za hadhi ya juu
Dar es salaam- Novemba 23, 2014 – kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua mpango maalumu utakaowawezesha wateja wake wakubwa kufurahia huduma za ziada wawapo kwenye kazi zao. Mpango huu wenye lengo la kuwazawadia wateja wa Airtel utakuwa na kadi maalumu ya kusafirisha yaani (Priority Pass) itayowawezesha wateja wakubwa wa Airtel kupata huduma ya hadhi ya juu kwenye viwanja vya ndege duaniani na pia kupata punguzo la hadi asilimia 30 pindi watakapo nunua bidhaa na kupata huduma nchini
Kufatia uzinduzi huo wateja wa Airtel sasa wataweza kuunganishwa na huduma za hadhi ya juu kwenye viwanja vya ndege zaidi ya 700 duniani na hivyo kupata viburudisho, urahisi wa huduma yaani (VIP services) pindi wasafiripo na kuwawezesha kufurahia safari zao
Sambamba na hilo wateja hao pia watapata punguzo la hadi asilimia 30 pale watakapopata huduma au kununua bidhaa katika maeneo mbalimbali ikiwemo hotel, migahawa, maduka makubwa and sehemu nyingine nyingi.
Akiongea wakati wa uzinduzi Waziri wa Nchini katika ofisi ya Waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dr. Mary Nagu alisema” nawapongeza sana Airtel kwa kuzindua mpango huu maalumu na kuwazawadi wateja na watanzania nchini. Nafurahi kuona pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya mawasiliano lakini bado tunashuhudia Airtel inajipanga na kujikita katika kuboresha huduma kwa wateja wake.
Natumaini kadi hizi maalumu tunazozindua leo zitawaweza watanzania kupata mwanya wa kutengeneza mahusiano na kutanua wigo wa marafiki wa kibiashara na mwisho kuweza kuvumbua fulsa mbalimbali za kibiashara duniani.”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema “ kupitia huduma hii tunadhirisha lengo letu la kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma zetu. Tunauhakika kadi hii maalumu ya kupata huduma zenye hadhi katika viwanja vya ndege mbalimbali duniani hazitarahisha safari zao tu bali zitawawezesha kufanya mahusiano ya muda mrefu ya kibiashara kwa wale watakaokutana nao wakati wa safari.
Ni matumaini yangu kuwa mpango huu utaleta tija na kuwapatia wateja wetu unafuu wa kutanua biashara zao,
Katika halfa hiyo Airtel pia ilizindua pia huduma yake ya internet ijulikanayo kama Home Wi-Fi solution,
kwa kupitia huduma hii ya Airtel Wi-Fi mteja anaweza kuunganisha simu zaidi ya 32 katika kifaa kimoja cha Wi-Fi , kuunganisha hadi simu za mkononi 4 na kuwaunganisha na Wi- Fi ya nyumbani hata kama wakiwa mbali na nyumbani wakati wote mahali popote nchini. Hii ina maana kwamba sasa wateja wa Airtel wanaunganishwa na kifaa kimoja cha familia , kwa kupitia kifurushi kimoja, kupitia huduma hii mpya ya Airtel Wi-Fi
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.