|
Mabingwa wa Safari Pool Afrika 2014 kutoka Afrika Kusini, timu ya Taifa ya Pool ya Nchi hiyo wakishangilia na kitita cha Dolla 5000$ sawa na pesa taslimu za Kitanzania Shilingi 8,500,000/= pamoja na medali za dhahabu baada ya kutwaa ubingwa huo uliojulikana kwa “Safari All Africa Pool Championship 2014” uliomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar esSalaaam. |
|
Rais wa Chama cha Pool Africa (AAPA), Saths Reddy (kulia) akimkabidhi Meneja wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini ya mchezo wa Pool, kitita cha Dolla 5000$ sawa na pesa taslimu za kitanzania 8,500,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyo malizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. |
|
Raiswa Chama cha Pool Africa (AAPA), Saths Reddy kulia) akimkabidhi Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo wa Pool kitita cha Dolla 2000$ sawa na pesa taslimu za kitanzania 3,400,000/= mara baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyo malizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam |
|
Wachezaji wa Taifa wa mchezo wa Safari Pool Tanzania, wakishangilia wakiwa na kitita cha Dolla 2000$ sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 3,400,000/= pamoja na medali za Silva mara baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwisho ni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. |
|
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool upande wa mchezaji mmoja mmoja (Singles), Ishmael Mthethwa kutoka Afrika Kusini akionyesha kitita cha Dolla 2,000$ sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 3,400,000/= pamoja na medali ya Dhahabu mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyo malizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo. |
|
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool upande wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) Wanaume, Ishmael Mthethwa kutoka Afrika Kusini akionyesha kitita cha Dolla 2,000$ sawa na pesataslimu za kitanzania Shilingi 3,400,000/= pamoja na medali ya Dhahabu mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. |
|
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool upande wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) Wanawake, Suzette Booyens (kulia) kutoka Afrika Kusini akionyesha kitita cha Dolla1,000$ sawa na pesa taslimu za kitanzania Shilingi 1,700,000/= pamoja na medali ya Dhahabu mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014”yaliyo malizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo. |
|
Msindi wa Pili waTanzania wa mchezowa Pool upande wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) Wanawake, Rose Deus (kulia) akionyesha kitita cha Dolla5,000$ sawa na pesataslimu za kitanzani Shilingi 850,000/= pamoja na medali ya Silva mara baada ya kuibuka msindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo. |
Na Mwandishi
Wetu.
AFRIKA
KUSINI MABINGWA SAFARI POOL AFRIKA 2014.
TIMU ya
Taifa ya mchezo wa Pool ya Afrika Kusini Wanaume imeibuka na ubingwa wa Afrika
katika mashindano ya Pool yaliyojulikana kwa “Safari Lager All Africa Pool
Championship 2014” yaliyofanyika katika Ukumbi wa Budget jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki na hivyo kujinyakulia zawadi ya Dolla 5,0000$ sawa na pesa
taslimu za kitanzani Shilingi 8,500,000/= pamoja na medali za dhahabu.
Mashindano
ya mwaka huu yaliendeshwa kwa mfumo wa
Ligi ambapo afrika Kusini walipata ubingwa kwa kuongozwa kwa Pointi 12,wakatiti
waandaaaji wa mashindano kwa mwaka 2014, Tanzania walipata pointi 10 na hivyom
kuzawadiwa dolla za kimarejkani 2,000$ pamoja na medali za silva wakifuatiwa na
Zambia mabingwa watetezi pointi 9ambao walikamata nafasi ya tatu na kuzawadiwa
medali za shaba, ambapo Uganda nafasi ya nne walipata pointi 7 na Kenya walipata nafasi ya tano kwa pointi 2.
Upande wa
Wanawake pia timu ya Afrika kusini ilitwaa ubingwa kwa pointi 11 na kuzawadiwa
medali za dhahabu, nafasi ya pili ilichukuliwa na Uganda kwa pointi 8 na
kuzawadiwa medali za silva, nafasi ya
tatu ilikwenda kwa Tanzania ambao walipata pointi 5 na Kenya ilikamata nafasi
ya nne kwa pointi 0.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanaume, IshmaelMthethwa kutoka Afrika Kusini alitwaa
ubingwa huo na hivyo kuzawadiwa dolla 2,000$ pamoja na Medali ya dhahabu wakati
mshindi wa pili ni Aden Joseph kutoka Afrika Kusini pia ambaye alizawadiwa
dolla 1,000$ pamoja na medali ya silva.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja(Singles) Wanawake, Nkosi Sikelel’l kutoka Afrika Kusini alifanikiwa kutwaa ubingwa
na hivyo kuzawadiwa dollah 1,000$ pamoja na medali ya dhahabu wakati
mshindi wa pili ni Rose Deus kutoka Tanzania ambaye alizawadiwa dolla 5,00$
pamoja na medali ya silva.
Akizungumza
na wanamchezo pamoja na wadau wa pool
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alishukuru kwa mashndano
kwanza kufanyika Tanzania kwa mara ya kwanza na pia alishukuru kwa mashindano
kuisha salama bila matatizo yeyote.
Shelukindo
aliipongeza timu ya Taifa ya Afrika Kusini kwa kutwaa ubingwa wa Afrika kwa
mwaka 2014 lakini pia aliipongeza timu ya Tanzania kwa kupiga hatua mpaka
nafasi ya pili upande wa timu na nafasi ya pili kwa kina dada singles.
Meneja Oscar
aliwaomba zwachezaji kuongeza juhudi katika mazoezi na ikiwezekana mwaka
ujao wa 2015 tuwe mabingwa wa Afrika kama ilivyo bia ya Safari Lager bia bora
Afrika.
Nae Rais wa
Chama cha Pool Afrika(AAPA), Saths Reddy aliipongeza Tanzania kwa makaribisho
mazuri na maandalizi mazuri na kukiri kwa mara zya kwanza mashindano ya Afrika
ya Mwaka huu 2014 yaliyoandaliwa na Tanzania yamekuwa na hamasa na ushindani wa
hali ya juu na hiyo inaonyesha kuwa mchezo wa Pool sasa umekuwa.
Mwisho Rais
aliwatakiwa kila nchi kurudi nyumbali salama na mashindano ya mwaka 2015
yatakuwa Lethoto hivyo aliwaomba Tanzania kupitia mzamini Safari Lager wasikose
kushiriki.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.