Topland Kinondoni mabingwa Safari
Pool 2014.
Na Mwandishi
Wetu.Moshi
KLABU ya Topland
ya Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni yenye makazi Magomeni jijini Dar es Slaaam
imefanikiwa kutetea ubingwa wa ke wa fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa
yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani Kilimanjaro kwa kuifunga timu ya
Anatory ya Mkoani Morogoro 13-3.
Timu ya
Topland kwa kutwaa ubingwa huo ilizawadiwa Kikombe,Medali za dhahabu na pesa
taslimu Shilingi 5,000 000/= wakati mshindi wa pili Anatory ya Morogoro
walizawadiwa pesa taslimu Shilingi 2,500 000/= pamoja na medali za fedha.
Mshindi wa
tatu katika fainali hizo ni timu ya Mashujaa kutoka Mkoa wa kimichezo wa Ilala
jijini Dar es Salaam ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 1,250,000/=
pamoja na medali za shaba wakati washindi wanne ni timu ya Mboya ya Mkoani
Kilimanjaro ambao ndio walikuwa wenyeji wa Mashindano hayo kwa mwaka 2014 ambao
walizawadiwa pesa taslimu Shilingi
750,000/=.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja Wanaume, Mussa Mkwega kutoka klabu ya Anatory ya Mkoani
Morogoro alitwaa ubingwa kwa kumfunga Innocent Sammy kutoka Mkoa wa kimichezo
wa Temeke 5-4 na hivyo Mkwega kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi
500,000/=,medali ya dhahabu pamoja na ngao wakati Innocent Sammy kwa kuchukua
nafasi ya pili alizawadiwa fedha taslimu shilingi 250,000/= pamoja na medali ya
fedha.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wakina Dada, Neema Hamis kutoka Mmkoa wa Tanga alitwaa
ubingwa kwa kumfunga Sada Tulla kutoka
Shinyanga na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 350,000/= pamoja na medali
ya Dhahabu wakati Sada Tullah yeye kwa
kukamata nafasi ya pili alizawadiwa pesa taslimu Shilingi 200,000/=
Akikabidhi
zawadi hizo Naibu Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia
aliipongeza Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya afari Lager kwa
kudhamini mashindano ya Pool Taifa na alliwaomba waendelee kufadhili kwani
mpaka sasa ni mchezo pekee ulioiletea sifa Nchi kupia fainali za Afrika ambapo
Mtanzania Patrick Nyangusi anashikilia Ubingwa wa Afrika.
Nkamia aliwataka
pia Chama cha Pool Taifa(TAPA) kutumia vyema fursa ya TBL kwa manufaa ya
kuendeleza mchezo huo nchini na Kimataifa na kwa jinsi hiyo aliwapa siku 60
wawe wameshafanya uchaguzi na kupata viongozi wa kuchaguliwa kikatiba na wa
muda tangu chama hicho kianzishwa kama ilivyo sasa.
Mwisho
Waziri Nkamia aliwatakia safari njema wanamichezo wote kurejea majumbani salama
na kuwaomba walichokipata kwa Safari Lager kama zawadi wakakitumie vyema kwa
maezndeleo yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.