ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 4, 2014

RAN IT SOLUTIONS YAPANIA KULETA MAPINDUZI KWENYE BIASHARA NAUTOAJI HUDUMA.

Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Ran IT Solutions (EA) LTD,  Lugumi Enterprises LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Afrika Mashariki yaliyoandaliwa na Chemba ya Biashara nchini TCCIA na kufanyika katika uwanja wa Nyamagana, jinsi kampuni yake ilivyo dhamiria kuimarisha utoaji huduma kwa njia ya mawasiliano ya teknolojia ya mitandao. MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY.


"Moja kati ya hatua muhimu kwenye biashara yoyote duniani ni utunzaji wa kumbukumbu hivyo wafanyabiashara wategemee kupata nyenzo zilizo na warrant na zenye ubora" Say's Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Ran IT Solutions (EA) LTD,  Lugumi Enterprises LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe,
Si katika Biashara tu pia tumeshuhudia mapinduzi makubwa katika utoa wa huduma za afya hapa nchini ambapo utoaji huo wa huduma huendana sanjari na uhifadhi wa taarifa mbalimbali ambapo  Kampuni ya Ran IT Solutions (EA) LTD imeweka mpango mkakati wa kuzifikia sekta zote katika utoaji wa vifaa vya utunzaji kumbukumbu vinavyodumu na vilivyo bora.
Mmoja kati ya maafisa wa mauzo wa Kampuni ya Ran IT Solutions (EA) LTD akitoa maelezo kwa mteja wake kwa lap top zinazouzwa kwenye banda lao uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Waandishi wa habari wakipata maelezo toka banda la Kampuni ya Ran IT Solutions (EA) LTD, lenye bidhaa makini zilizo madhubuti kwenye soko la sasa linalomtaka kila mwananchi kwenda na wakati.
Mmoja kati ya maafisa wa mauzo wa Kampuni ya Ran IT Solutions (EA) LTD akizianisha baadhi ya bidhaa za kielektroniki zilizopo ndani ya banda lake, kuanzia wino wa mashine za uchapaji, kompyuta na visaidizi vyake, kamera za aina zote na bidhaa nyingine za kielektroniki. 

Katika Maonesho haya ya TCCIA wadau mbalimbali wamejikita kutangaza bidhaa wanazozalisha ambapo hapa nikatika banda la ORYX.
Mambo ya urembo na virembesho ni katika banda la Tressa.
Masuala ya pembejeo za kilimo.
Mbegu.
Mambo ya urembo na nakshi za ngozi.
Matrekta kwaajili ya kilimo cha kisasa.
Shirika la Hifadhi ta Taifa nchini TANAPA ndiyo washindi wa jumla katika Maonesho ya 9 ya Biashara Afrika Mashariki ya TCCIA yanayofanyika uwanja wa Nyamagana jijii Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.