ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 18, 2014

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AOMBA SAPOTI YA KUANDALIWA MECHI YA KUTETEA MKANDA WAKE WA WPBF AFRICA


Na Mwandishi Wetu
 BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe'won 11 (KO 4) + lost 1 (KO 0) + drawn 0 = 12  anayeshikilia mkanda wa WPBF Africa katika uzito wa light welterweight amejitokeza hadharani na kusema kwamba mchezo wa ngumi nchini Tanzania haulipi kutokana na malipo yake kuwa madogo. Huyu ni bondia aliyefanikuwa kuwa bingwa baada ya kumpiga Mwansa Kabinga
Mpambano ulio fanyika  june 8 mwaka huu huko  Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia na kuibuka mshindi katika raundi ya tisa bondia huyo mwenye ndoto ya kuwa bingwa wa dunia katika miaka ya hivi karibuni.



Amesema mabondia wa hapa nchini bado hawajajielewa kutokana na kuto kuwepo na wafadhili wa kutosha katika mchezo wa masumbwi ila ufadhili mwingi unapelekwa katika mambo ya soka huku wakiuwacha mchezo wa masumbwi ukiwa hauna mwelekeo na sapoti yoyote.

Bondia huyo alijitamba  kwa kujinasibu kuwa kwa hapa nchini hakuna bondia ambaye anaweza kumbabaisha katika kipindi hiki kwani yeye kwa sasa yupo matawi ya juu.

Bondia huyo anayefanya mazoezi katika kambi ya Ilala ananolewa na jopo la makocha likiongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D', amewaomba watu mbalimbali kujitokeza kumsaidia ili kutetea mkata wake wa WPBF Africa alioupata Zambia ili awadhilishie watu kuwa uwezo alionao ni mkubwa sana katika masumbwi.

Pia amewataka wadhamini kujitokeza kumpa sapoti kwani ana uwezo wa kuwatangazia biashara mbalimbali ukizingatia yeye ni bingwa na bado kijana mdogo mwenye nia ya kufika mbali katika mchezo wa masumbwi nchini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.