Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imewawezesha wakazi wa kijiji cha Aicho na vijiji vya jirani kupata huduma za mawasiliano kufatia uzinduzi wa mnara wa mawasiliano katika kijiji cha Aicho kata ya Marang wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara
Uzinduzi huo ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel katika kuboresha upatikanaji wa mawasiliano na kuwawezesha wakazi wa maeneo ya pembezoni mwa nchi kupata huduma ya mawasiliano ya simu za Mkononi
Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika mkoani Manyara Meneja Mauzo kanda ya kaskazini wa Airtel Bwana Brighton Majwala alisema “ Airtel Tunatambua kuwa mawasiliano ni kichocheo kikuu cha uchumi katika nchini na jamiii yoyote ile, ndio maaana tumeona ni vyema kufikisha mawasiliano katika maeneo yenye changamoto za mawasiliano hususani ya vijijini.
Na leo tunazindua huduma za mawasiliano katika kijiji cha Aiko na kuwawezesha wakazi wa hapa na maeneo ya jirani kupata huduma mbalimbali ikiwemo za kifedha za kutuma na kupokea pesa, kufanya malipo kwa njia rahisi, salama wakiwa mahali popote kwa kupitia huduma ya Airtel Money”. “Airtel tumejipanga na tutaendelea kutekeleza dhamira yetu ya kutoa huduma bora za kibunifu na za bei nafuu na huku tukiendelea kuboresha upatikanaji wa mawasiliano katika maeno mbalimbali ya pembezoni nchini” aliongeza Majwala
Kwa upande wake mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbulu Joseph Geheri alisema” Tunashukuru sana Airtel kwa kuendelea kuboresha mawasiliano na kuwapa vijana wetu kufaidika na kupata Ajira kwa kupitia huduma hizi zilizosheheni hapa wilayani Mbulu.
Kadhalika mawasiliano haya yamewawezesha wanafunzi kupata taarifa za matokeo yao ya mtihani ya kuhitimu kwa kupitia simu za mkononi mahali popote pale walipo.
Vilevile tunafurahi kuona jinsi gani Airtel imerahisha mawasiliano haya kijiji hapa na kuwezesha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wakati na kirahisi zaidi, kwa wafanyabiashara, wakulima pamoja na wafugaji mawasiliano haya yatawawezesha kuendesha shughuli zao za kiuchumi kwa ufanisi zaidi na kupata masoko katika sehemu mbalimbali za nchi kupitia mtandao huu wa simu za mkononi wa Airtel.
Nachukua nafasi hii kuwaasa wakazi wa hapa kuyatumia mawasiliano haya kwa faida ya maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla Aliongeza Geheri
Airtel inaendelea kupanua wigo wa mawasilano nchini ambapo wiki zilizopita Airtel ilizindua mnara wa mawasiliano katika mkoa wa Sigunga Kigoma na Muhukuru Songea , huku ikiwa na mpango mkakati wa kuzindua huduma za mawasiliano katika maeneo mengi zaidi nchini.
Sasa wakazi wa sigunga, Mahukuru na Aicho wanafurahia huduma mbalimbali za Airtel ikiwemo ya kifedha ya Airtel Money Hatoki Mtu hapa, Switch on huduma ya internet na vifurushi vya Airtel yatosha na vingine vingi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.