ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 22, 2014

DKT. KAMANI AMUKUNA WAZIRI MKUU PINDA AMUUNGA MKONO KWA UJENZI WA KITUO CHA ALBINO.








NA PETER FABIAN,
BUSEGA.
 
MBUNGE wa Jimbo la Busega mkoani Simiyu Dkt Titus Kamani adhamiria kuokoa maisha ya walemavu wa ngozi (Albino) baada ya kusaidia ujenzi wa kituo cha watoto wenye ulemavu eneo la kijiji cha Bukungu jimboni humo.

Hatua hivyo inatokana na vitendo vya mauaji ya kikatili kwa Albino vinavyokuwa vinafanyika wilayani humo na kumsukuma Dtk.Kamani, kuanzisha ujenzi wa kituo hicho cha kulelea watoto wenye ulemavu huo.
 
Kituo hicho kinachojengwa Kijiji cha Lukungu, Kata ya Lamadi, kitakachokuwa na uwezo wa kuchukua watoto zaidi ya 100, kinataraji kugharimu zaidi ya sh Bilioni 1.5 hadi kukamilika kwake.
 
Mbunge katika juhudi zake hizo za kuokoa maisha ya walemavu hao, zimeungwa mkono na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambaye ameatoa kwa kuunga mkono kwa kuchangia kiasi cha sh milioni 5 kwa ajili ya kuongeza kasi ya  ujenzi ambao tayari umeisha anza na unaendela na unatarajiwa kukam ilika Agosti mwaka kesho.
 
Akizungumza katika eneo la ujenzi huo ambao umefikia hatua ya msingi jana, Dk Kamani alisema hali hii imenisukuma kwa moyo wa dhati kuhakikisha ujenzi huu unakwenda kwa kasi “lakini vitu ambavyo navifikiria sana na ningependa niondoke madarakani nikiwa nimevikamilisha, ni pamoja na kituo hiki cha walemavu.”alisisitiza
 
Aidha aliongeza kuwa hapa sisikilizi la mtu lazima kituo hiki kiishe na sitaki kiwe cha ujanja ujanja, namshukuru sana mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye pia ni mlezi wa walemavu hao kuguswa na jitihada zangu na kuniunga mkono kwa kunichangia sh Milioni 5 zilizotolewa na Waziri Mkuu Pinda .
 
Alieleza kwamba, amekuwa akijishughulisha na makundi yaliyosahaulika hasa ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambao nao ni sehemu ya jamii hivyo kituo hicho pia kitalea watoto wenye ulemavu wa viungo na macho, anaomba taasisi mbalimbali, watu wenye uwezo na wananchi wa eneo hilo wamuunge mkono ikiwa pamoja na kuwa walinzi wa watoto hao.
 
“Kampuni ya saruji ya Twiga tayari imetupatia mifuko 600 ya saruji iliyoanzisha ujenzi huo, imepaswa kuwa mfano bora wa kuigwa na yeye binafsi anagharamia fedha za kulipa mafundi, uchoraji wa ramani na usajiri wa kituo hicho ambacho kitaitwa Mother Thereza Albinus Disability Hope Centre,”alisema
 
Kwa upande wake Mratibu wa Kituo hicho Moody Gimonge alisema kwamba, kitakapokamilika kitaanza kwa kuchukua walemavu wa wilaya ya Busega wanaolelewa katika vituo vya Shule ya Msingi Mwisenge mkoani Mara, Buhangija mkoani mkoani Shinyanga na katika sehemu nyingine za wilaya hiyo.

Mratibu huyo alieleza kwamba, anasikitishwa kuona watu wengi wanaanzisha vituo hivyo kwa ajili ya maslahi yao binafsi badala ya kuwa na dhamira ya dhati ya kuwasaidia walemavu hao kama Dk Kamani alivyo dhamiria na ni Mbunge anayetimiza ahadi yake ya kusaidia jamii ya walemavu wakiwemo Albino.
 
Wito wangu kwa jamii iondokane na imani za kishirikina na mira potofu kwamba viungo vya Albino vinaweza kumpatia mtu utajiri wakati familia zao zilizozaa watoto hao zikiwa bado maskini hivyo kuwajengea tu vituo haitatosha bali jamii ielimike na kuchukua jukumu la kuwalinda na kuto wanyanyapaa kwani ni sawa na binaadamu wengine.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.