Meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula (katikati) akipiga teke kibendera cha kona za uwanja kama sehemu ya kupima ubora wa vitendea kazi vya mashindano ya Pepsi Kombe la Meya 2014. |
Daladala. |
Igoma. |
Pamba. |
Mnadani. |
Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula akizungumza na wanahabari. |
TIMU 22, Waamuzi na Kamati ya Maandalizi jana wamekabidhiwa vifaa na vitendea kazi kwa ajili ya kuanza rasmi mashindano ya ya Pepsi Kombe la Meya wa Jiji la Mwanza 2014 jijini Mwanza.
Akikabidhi vifaa na vitendea kazi hivyo, Meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula (CCM) ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mkolani alisema kwamba licha ya mashindano hayo kuwa na dhamira ya kukuza vipaji na kipato kwa wajasiliamali vijana kupitia zawadi kwa washindi, pia mashindano hayo yamelenga kujenga udugu,urafiki na mshikamano miongoni mwa wananchi wa jiji la Mwanza.
“Tutumie vizuri fursa hii hasa vijana kwa kucheza na kuzingatia kanuni na sheria za mashindano ili kupata ushindi utakaowezesha timu kupata zawadi ili kuwezesha kuwa na mtaji wa kujiendeleza katika ujasiliamali na vifaa hivi vitatolewa tena kwa timu zitakazoingia robo fainali na fainali ikiwa ni uboreshaji kwa mwaka huu,”alisisitiza.
Kwa upande wake Meneja wa Masoko wa Kampuni ya SBC Sharif Taki inayodhamini mashindano hayo kwa mwaka wa pili mfululizo kupitia kinywaji chake cha Pepsi alisema kwamba, mashindano ya mwaka huu wameboresha zaidi udhamini wao kwa kuongeza timu kutoka timu 19 hadi kufikia 22 ikiwemo zawadi kwa washindi, ubora wa vifaa na vitendea kazi, huku michuano hiyo ikichezeshwa na waamuzi wanafunzi wa Kituo cha Soka cha Alliance cha jiji Mwanza.
Timu zilizokabidhiwa vifaa ikiwa ni seti kamili ya jezi, mipira miwili pamoja na nauli ya kufika katika kituo wakati wa mechi Sh.20,000 ambayo hutolewa siku timu inacheza, timu za Kata ya Mbugani, Nyamagana, Mkolani, Buhongwa, Butimba, Igogo, Mkuyuni, Mirongo, Pamba, Igoma, Isamilo na Mahina zile za Vikundi na Taasisi ni Magazeti FC, Wanahabari FC, Pilisi Jamii FC, Bodaboda, Sokoni, Mnadani, Fundi Gereji, Mwanza City FC, Machinga FC na Daladala FC.
Mashindano hayo yanayosimamiwa na Kampuni ya Myway Entartainment, yanataraji kuzinduliwa rasmi Agosti 2 Mwaka huu katika uwanjwa wa Nyamagano ambapo timu za Kata za Mkolani na Isamilo (Mabingwa) zitafungua dimba kabla ya timu zingine kuchuana katika viwanja vya Mabatini Polisi, Igoma, Mkolani, Buhongwa na Nyegezo kona ambapo timu zinetengwa katika makundi manne ambapo makundi ya A na C yatakuwa na timu sita na B na D yatakuwa na timu tano kila moja.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.