ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 9, 2014

Qatar KWENDA KORTIN KUHUSU 2022.

Qatar yatafakari kwenda Mahakamani kutetea uwenyeji wa Kombe la dunia QATAR 2022

Maafisa wa Qatar wanaaminika kupanga mikakati madhubuti ya kukabiliana na tishio la kupokonywa uenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa Qatar 2022 kufuatia tuhuma za rushwa .
Kamati andalizi ya michezo hiyo sasa inaaminika kupania kufanya kila iwezalo ikiwemo kufuata mkondo wa kisheria, ikiwa kura ya kuchagua mwandalizi wa kombe la dunia 2022,itarudiwa.

Shutuma za ufisadi katika mchakato wa kupiga kura ya uwenyeji zilisababisha kuitishwa kwa kura nyingine ikiwa hila itaonekana kuwa ilifanyika.
Rais wa Fifa akwepa maswali kuhusu hongo katika uteuzi wa Qatar 2022
Qatar inakana shutma za hongo.
Hata hivyo hatma yake imo mikononi mwa mchunguzi wa FIFA,Michael Garcia.
Mwanasheria huyo kutoka Marekani anatarajiwa kukamilisha uchunguzi wake itimiapo Juni 9.


Pauni bilioni 23 zimetumika tayari nchini Qatar
Rais wa Uefa, Michel Platini, aliyeipigia kura Qatari, alisema kuwa atakubali kufanyike kura ya marudio iwapo shutma za ufisadi dhidi ya Qatari zitathibitishwa.
Msimamo wake uko sawa na ule wa makamu wa rais wa Fifa, Jim Boyce aliyesema kuwa hatakuwa na shida yoyote ikiwa ‘makubaliano yatakuwa ni kura ya marudio kufanywa.’

Maafisa wa Qatari wanadai kuwa mtaji wa takriban pauni bilioni 23, mahsusi kwa ajili ya kombe la dunia la 2022, itapotelea mbali iwapo Fifa italipokonya taifa hilo la ghuba haki ya kuandaa michezo hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.