Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo wakati akitoa salamu za Mkoa huo wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya siku ya maadhimisho ya mazingira duniani yaliyozinduliwa Juni 2 mwaka huu na Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Binilith Mahenge, ambapo kitaifa yanaadhimishwa jijini hapa.
Mhandisi Ndikilo alieleza kuwa, athari hizo za uharibifu wa mazingira zimesababisha pia kupotea kwa vyanzo vya maji safi na salama katika baadhi ya maeneo ya mkoani humo hali ambayo imepelekea kupotea kwa makazi ya viumbe hai mkoani humo.
Katika kukabiliana na hali hiyo Mkoa wa Mwanza umechukua hatua mbalimbali ikiwemo upandaji miti kwa asilimia 78, kutoa elimu juu ya hifadhi ya mazingira kwa njia ya vikao, semina, makongamano na maadhimisho ya kimkoa na kitaifa, kusimamia sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kutunga sheria ndogo na kuzitekeleza.
Aliongeza kuwa hatua zingine ni kuhamasisha matumizi ya Nishati mbadala kama gesi na umeme jua, kuhamasisha shughuli za ujasiriamali zinazotoa ajira mbadala kama vile ufugaji nyuki, samaki na utalii katika visiwa na mwambao wa Ziwa Victoria, kuanzisha utaratibu wa usafi kwa kila wiki ya kwanza ya mwezi na kuwachukulia hatua wanaokaidi sheria zilizopo.
Aidha Mkuu huyo aliwataka wananchi wa Mkoa huo katika maeneo yao kuwa tayari kushirikiana na viongozi na watendaji wa Serikali ambao watatoa ushauri kwa jamii juu ya usafi na uhifadhi wa mazingira watakapowafikia.
“Mkoa unakabiliwa na changamoto ya ukame katika maeneo ya Wilaya za Kwimba, Magu na Misungwi, pia uvunaji miti kiholela kwa ajili ya mbao na mkaa, uvuvi haramu kwa kutumia sumu na vyavy haramu, uchimbaji holela wa madini, uvamizi wa maeneo ya mistu kwa ajili ya kilimo, makazi na ufugaji hali hii imeharibu mazingira,”alisema.
Huku Waziri Mahenge akiwataka wananchi nchini kote kutumia nishati mbadala ya jua, upepo na biogesi ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, kutumia majiko banifu yanayotumia kuni chache, kupanda miti kwa wingi, kudhibiti uchomaji moto ovyo, wamiliki wa viwanda wazingatie matumizi ya nishati zisizoongeza gesijoto angani na kilimo chenye kuzingatia matumizi bora ya ardhi.
Burudani ya ngoma ikitawala. |
Kula kitu nyoka balaaa!!. |
Ameingia wapi tena ayaaaaaa!! Akila mzigo utamlaumu nani? |
Manjonjo kwenye burudani.... |
Nyoka alipopelekwa jukwaa kuu kila Mhe. ilibidi ajisalimishe kwa kuingia mfukoni na kutoa mkwanja aka 'umateumate'. |
Hata nyoka wadogo ni balaaa... si unakumbuka ule msemo mtoto wa Nyoka naye ni Nyoka. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.