ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 3, 2014

ZAIDI YA KAYA 75 MWANZA ZATHIBITIKA KUTIRIRISHA VINYESI KWENYE MITO INAYOINGIZA MAJI ZIWA VICTORIA

WAKATI Rais Dkt. Jakaya Kikwete anataraji kuwa mgeni rasmi wa kilele cha siku ya maadhimisho ya mazingira duniani yanayoadhimishwa kitaifa Juni 5 mwaka huu mkoani Mwanza, uchafuzi wa mazingira mto Mirogo umeongezeka jijini hapa.


Imebainika kuwa, Kaya 75 jijini humo zinatirilisha vinyesi na majitaka ndani ya Mto Mirongo unaomwaga maji machafu Ziwa Victoria hali ambayo imedaiwa kuongezaka kwa kasi ya uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa mto huo hivyo kuhatarisha afya watumiaji wa maji ikiwemo wanyama, mimea na viumbe hai waishio majini.
Hali hiyo pia ilijitokeza na kushuhudiwa na baadhi ya wadau wa mazingira kutoka Menejimenti ya Ofisi za Maji Bonde la Ziwa Victoria, Maafisa Afya wa Jiji la Mwanza na Jumuia ya waumiaji wa maji na mazingira walipokuwa wakifanya zoezi la kufafisha mto Mirongo hii leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yanayofanyika jijini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la daraja la Mabatini linalopitiwa na mto huo baada ya kubaini kuwepo kwa Kaya hizo, Kaimu Afisa wa Maji kutoka Bonde la Ziwa Victoria Godfrey Kajanja alisema kwamba, Ofisi yake na Halmashauri ya Jiji zitakutana kuchukua hatua za kisheria kwa Kaya hizo na watu walio na tabia ya kuchafua maji ya mito.
Kajanja alisema kwamba, hali hiyo ikiachwa kuendelea bila kudhibitiwa kutawezesha kuibuka magonjwa ya tumbo endapo Mamlaka ya Majisafi na Mazingira ya jijini humo haitachukua hatua za kuongeza kiasi kikubwa cha dawa ya kutibu maji kabla ya kusambazwa kwa watumiaji.
“Lazima sasa tushirikiane kuzitekeleza sheria zilizopo za Mipango miji kwa upande wa Jiji la Mwanza, pamoja na ofisi yetu ya Bonde kutumia sheria ya usimamizi wa rasilimali ya maji Na. 11/2009 na sheria ya usimamizi wa mazingira Na. 24/2004 ambazo zinaoanisha adhabu ya fedha na kifungo kwa watu watakaokaidi na kukutwa na makosa,” alisema.

Kwa upande wake Mhandisi wa Maji toka ofisi za Bonde la Ziwa Victoria Mhandisi Jane John alieleza kwamba, hatua hivyo inatakiwa kukomeshwa mara moja na jamii iliyo kandokando ya maeneo unapipita mto Miringo na maeneo ya vyanzo vya maji ili kusaidia kulinda na tabia ya uchafuzi wa mazingira ikiwemo udhibiti jambo ambalo litaepusha uharibifu na uchafuzi.
“Tumeshuhudia mabomba ya vinyesi na maji machafu yakimwaga mtoni wakati tukifanya usafi wa pamoja kwenye mto Mirongo na wadau mbalimbali walioko kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira kitaifa hili ni jambo ambalo linahitaji hatua za haraka kulikomesha na kuwachukulia hatua wanaofanya uchafuzi huu,”alisisitiza.

Naye Mwenyekiti wa NGO ya Jumuiya ya watumiaji maji na mazingira Adam Shija ya Kata ya Mbugani Wilayani Nyamagana mkoani hapa alisema kwamba, tumekuwa na changamoto kubwa wakati wa usafishaji wa mto huo na wamebaini kuwepo kwa baadhi ya Kaya 75 ambazo zimekuwa zikitirilisha uchafu wa vinyesi na majimachafu ndani ya mabomba yaliyoelekezwa mtoni humo.
Shija alifafanua walipotembelea kandokando yam to huo kwenye maeneo ya unapoanzia na kupitia kasha kumwaga maji ziwani Victoria katika Kata za Nyakato walibaini kaya 16, Mahina kaya 8, Mbugani kaya 24, Mirongo kaya 17, Nyamagana kaya 6 na Pamba kaya 4 na tayari orodha hiyo imetokana na ukaguzi wa Jumuiya hiyo hivi karibuni.
Wito wangu kwa Serikali na Idara zenye jukumla la kusimamia rasilimali ya maji na mito, mabwawa na ziwa Victoria kutekeleza sheria kwa vitendo ili kukomesha tabia hiyo ya uchafuzi wa maji na uharibifu wa mazingira unaofanywa kwa makusudi na baadhi ya wananchi bila kujali kama husababisha madhala kwa watumiaji wa maji na kuhatarisha uhai wa viumbe hai majini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.