ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 23, 2014

KIKUNDI CHA NGOMA CHA RUGU - KARAGWE CHATWAA UBINGWA WA MKOA BALIMI NGOMA KAGERA.

Kikundi cha Ngoma cha Rugu- Karagwe  chatwaa ubingwa wa Mkoa Balimi Ngoma Kagera.
Na Mwandishi Wetu.
FAINALI za mashindano ya Ngoma za Asili  ngazi ya mikoa zijulikanazo kama “Balimi Ngoma Festival 2014” Mkoani Kagera kikundi cha Rugu chenye makazi yake Karagwe kimefanikiwa kuwaa ubingwa wa Mkoa wa Kagera  na kuzawadiwa fedha taslimu Shingi 600,00/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Kagera katika fainali za Kanda zinazotarajiwa kufanyika Augusti 16,2014 Mkoani Mwanza.
Nafasi ya pili ya mashindano hayo ilichukuliwa na Kikundi cha Rugoloile cha mjini Bukoba ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa katika fainali za Kanda.
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Abagambakamo cha Muleba  ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= na nafasi ya nneilichukuliwa na kikundi cha Alute Continue ambacho kilizawadiwa fedha taslimu shilingi 300,000/=.
Nafasi ya tano mpaka ya mkumi ilichukuliwa na Uviti Ruzinga,Chupukizi,Kasharu,Kabete cha Ihangilo,Jipe Moyo na Upendo Musira hivi vilizawadiwa kifuta jasho cha 150,000/= kila kikundi.Jumla ya Vikundi 11 vilijitokeza kushiriki fainali hizo za Mkoa wa Kagera ngazi ya Mkoa kwa Mwaka 2014.
Akizungumza na kwa nyakati tofauti Meneja matukio wa Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela alisema Sababu msinigi ya kuwepo kwa Mashindano ya Balimi Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania.
Mwayela aliongeza pia kuwa wao Kampuni ya Bia nchini ni sehemu yao ya kurudisha fadhila kwa watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra Lager pamoja na vinywaji vyote vya Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).

Fainali za Mkoa wa Kagera zilifanyika katika Uwanja wa Mkoa wa Kaitaba na fainali za Kanda za mashindano ya Balimi Ngoma zinatarajiwa kufanyika August 16,2014 jijini Mwanza kwa kushilikisha vikundi viwili viwili kutoka Tabora, Shinyanga, Bukoba, Musoma na Wenyeji wa mashindano Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.