ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 6, 2014

ALICHOSEMA KOMBA LEO KWENYE PB MARA BAADA YA PICHA ZA KUCHAFULIWA MITANDAONI.

Imekuwa ni siku ngumu leo kwa Mhe. Komba, hali iliyosababisha kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi kushindwa kabisa hii leo kuhudhuria vikao mbalimbali vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vinavyoendelea mjini Dodoma.

Hali hiyo imekuja mara baada ya picha mbalimbali chafu kusambazwa kwenye mitandao zikimuonyesha kiongozi huyo akijiachia katika hali ya kingono na binti mmoja ambaye hata hivyo jina lake halijajulikana.

Power Break Fast ya Clouds Fm hii leo kupitia mwakilishi wake mjini Dodoma (Special kwa masuala ya Bunge) Simon Simalenga, imefanya juhudi hatimaye kufanya mahojiano na kiongozi huyo kupata maoni yake juu ya shutuma hizo nzito dhidi yake.
IFUATAYO NI SAUTI YA MHE. KOMBA (BOFYA PLAY KUSIKILIZA) 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.