ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 22, 2014

UMATI- “KUPIGA HODI BUNGENI”

Mkurugenzi wa UMATI nchini Bi. Lulu Ng'wanakilala, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokutana nao katika Hotel ya Ryans Bay jijini Mwanza.
Bibi Pamela Msei Meneja wa UMATI kanda ya Ziwa.
Ni, Picha ya pamoja mara baada ya kikao na waandishi wa habari.
UMATI- “KUPIGA HODI BUNGENI”
·      Ni kwenda kutete bajeti za Wizara husika.
CHAMA cha uzazi na malezi bora nchini UMAT, Tanzania kimeazimia kwenda Bungeni Mjini Dodoma kwa ajili yakuwakilisha mambo mbali mbali yanayo kikabili chama hicho, ikiwapo kuongea na mlezi wao ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiongea na vyombo vya habari Jijini Mwanza mkurugenzi mtendaji wa UMAT Tanzania, Lulu Ng’wanakilala, alisema kama UMAT wanadhamiria kwenda Bungeni wakati Wizara zinazohusika na masuala ya uzazi na Malezi zitakapokuwa zikiwasilisha bajeti zao za mwaka 2014/2015 ili kuweza kuwashawishi wabunge waweze kuziongezea Wizara hizo bajeti yakutosha kwa ajili yakufikia malengo ya Milenia katika masuala ya uzazi wa mpango, ambapo lengo ni kufikia asilimia 60% ifikapo 2015. “Tunadhamiria kwenda Bungeni na kuonana na wawakilishi wa wananchi, tukiwa na lengo la kuimba Serikali kuziwezesha Wizara ambazo zinahusika na masuala ya Uzazi kwa ujumla ili ziweze kutengewa fedha za kutosha katika bajeti ijayo ili tuweze kufikia malengo ya Milenia” alisema na kuongeza “ kwa hivi sasa kiwango cha matumizi ya uzazi wa mpango ni asilimia 27% na lengo letu nikufikia aslimia 60% jambo ambalo unaona tunakazi ya ziada sana kufikia hatua hiyo” aliwaambia waandishi wa habari waliokuwa wanazungumza nao katika Hoteli ya Rayanzi Bay ya Jijini Mwanza.
Katika hatua nyingine, Ng’wanakilala, alisema katika mataifa Mengine suala la uzazi wa mpango limekuwa linauwakilishi rasmi jambo ambalo linasaidia kurahisisha shughuli hizo kwenda vizuri na sekta husika kutengewa mafungu yakutosha.
UMAT ambayo imekuwa ikijishughulisha na masuala ya uzazi wa mpango, inakabiliwa na changamoto nyingi katika vita hivyo, ikiwamo mila potofu zilizopo kwenye jamii kama vile mwanamke kufanywa chombo cha uzazi hivyo muda mwingi kubakia katika suala la kuzaa na kulea na hivyo kukwamisha hata shughuli za uzalishaji mali.
Katika hatua nyingine UMAT, imesema Mikoa ya kanda ya ziwa inayounganisha mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Geita, Simiyu na Shinyanga ndio yenye Changamoto kubwa zaidi kwani hadi hivi sasa ni asilimia 13% ya jamii ndiyo inayo zingatia masuala ya uzazi wa mpango ikilinganishwa na wastani wa kitaifa wa asilimia 27% huku lengo la kitaifa likiwa ni asilimia 60% ifikapo 2015, hivyo kuifanya UMAT kuelekeza nguvu kubwa katika kanda hiyo kwa kuanzishwa kwa Mradi mpya wa Water Lou, ambao umekusudia kufanya kazi katika Mkoa wa Mara.
UMATI ambayo ilianzishwa mwaka 1959, imekuwa ikijihusisha na masuala ya uzazi wa mpango kwa Jamii ya watanzania ambao kabla ya Uhuru Idadi ya wanachi wakti huo walikuwa Milioni 9, huku idadi ya sasa ikifikia milioni 45 na zaidi na kukifanya chama hicho kuongeza juhudi katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na uzazi salama ili kuweza kumfanya mama naye aweze kuingia katika shughuli za uzalishaji mali. .
Imeandaliwa na: Atley Kuni- Afisa habari na Mawasiliano Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.