TOUCH FOUNDATION KUENDELEA KUSAIDIA SEKTA YA AFYA TANZANIA
Na Mwandishi Maalum
Touch Foundation ,Taasisi isiyo ya kiserikali na yenye makao yake nchini Marekani, mwishoni mwa wiki ( Mei 8),
imeadhimisha miaka kumi ya kazi zake na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya
Tanzaniana Taasisi nyingine katika uboreshaji na uimarishaji wa sekta ya afya nchini.
Katika hafla iliyojulikana kama Asante
Supper 2014,
ilihusisha pia utoaji wa tuzo kwa wadau mbalimbali ambao wamekuwa nguzo muhimu ya Taasisi hiyo.
Asante Supper
ilihusisha pia harambee ya uchangishaji wa fedha kwa ajili ya kusaidia sekta hiyo ya afya. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Morgan Library Museum, Jijini New York.
Akiwakaribisha wageni waalikwa, Rais wa Touch Foundation, Lowell Bryan
pamoja na kuelezea mafanikio ya taasisi yake iliyoanzishwa mwaka 2004 katika uboreshaji wa sekta ya afya nchini
Tanzania, amewataka wafadhili mbalimbali kuendelea kujitolea na kuchangia zaidi ili sekta ya afya nchini
Tanzania iweze kuimarika na hatimaye kumaliza au
kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo.
Akasema utashi wa kisiasa na wa kiuongozi ambao Mh.Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha katika, situ kutambuana kuthamini mchango wa
Touch Foundation na Taasisi nyigine kama hiyo,
bali pia amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba sekta ya afya inaimarika nchini
Tanzania na huduma za afya zinawafikia wananchi kule walipo.
Naye Padre Dkt. Peter le
Jacq ambaye naye amekuwa na mchango mkubwa wa uimarishaji wa sekta ya afya nchini kupitia Hopistali ya Bugando anaambaye haswa ni chimbuko la Touch
Foundation, hakusita kutoa shukrani zake kwa Rais Kikwete na kumuelezea kama kiongozi anaye jituma, kujitolea na mwenye ushirikiano mzuri za sekta binafsi.
Katika Miaka kumi ya uhai wake Touch Foundation imekuwa ikishirikiana na kufanya kazi kwa Karibu na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
na hususani Chuo Kikuu cha Kikatoliki
cha Afya na Sayansi Mwambata cha Bugando (CUHAS).
Ushirikiano huo unahusisha katika maeneo mbalimbali mtambuka yakiwamo mafunzo ya madaktari na wataalam wa fani mbalimbali kupitia
CUHAS na hivyo kuchagia ongezeko la madaktari na wataalam.
Mbali ya watendaji wakuu wa Touch Foundation, wakiongozwa na Rais wake, Bw. Lowell Bryan, pamoja na wafadhili. Asante
Supper 2014 ilihudhuriwa pia na wageni maalum kutoka Tanzania na ujumbe huo ulihusisha Muhashamu Thaddaeus Ruwa’ichi Askofu Mkuu wa Mwanzana Mwakilishiwa Kudumu wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi alikuwa miongoni wa wageni waaalikwa.
Wengine kutoka
CUHAS walikuwa ni Askofu Augustine Shao,
Makamu Mkuu wa CUHAS , Profesa Jacob
Mtabaji, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Augustine, Padre Dkt. Charles
Kitima, Profesa Paschalis Rugarabamu, Dkt, IsidorNyahomela, Dkt. Frederick
Kigadye, Dkt. Charles Majinge, Dkt.
Manage Manyama, Dkt. Stella Mongella,
Dkt. Godwin, Godfrey Sharauna Sister Marie- Jose Voeten kutoka hospitali Teule ya Sengerema.
Baadhi ya Madaktari hao kutoka Bugando na hasa wale
walio nufaika na ufadhili wa Touch Foundation walielezea walivyo nufaika na ufadhili
huo ambao umewawezesha kusoma, kujipatia ujuzi na hivyo kupata fursa ya kuwahudumia
watanzania wenzao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.