Mwigizaji na Mchekeshaji ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Bongo Movie Unity, Steven Mengere 'Steve Nyerere' (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juzi baada ya kuteuliwa kuwa msimamizi wa mkuu Wasanii wa nje ya Bunge Maalum, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Kwanza nje ya bunge, Renatus Muadhi, na katikati ni Mwenyekiti wa Taasisis hiyo, Agustino Matefu. |
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
WASANII wa Bongo Movie, muziki wa dansi, taarab, maigizo na tamthilia wametangaza kuzunguka nchi nzima wakiwa na kamati ya Tanzania Kwanza Nje ya Bunge Maalum la Katiba kwa lengo la kutangaza amani kwa vijana wa rika lote bara na visiwani.
Baadhi ya wasanaii hao ni pamoja na Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ ambaye ameteuliwa kuwa msimamizi mkuu wa uwakilishi kwa upande wa wasanii katika Tanzania kwanza nje ya Bunge maalum, Muungano huo uko chini ya Mwenyekiti Augustino Matefu.
Akizungumza juzi na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Steve amesema kwamba ataungana na wasanii ambao wako katika vyama mbalimbali kama vile Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, NCCR, Mageuzi , Cuf na vyama vingine huku wote wakiwa na lengo moja tu la kuhimiza mchakato wa katiba uendelee huku wanasiasa wakizingatia kudumisha amnai na umoja wa Watanzania.
Nyerere aliongeza kwa kusema kuwa yeye hakuwa na kipingamizi pindi alipoambiwa amechaguliwa kuwa miongoni mwa wasimamizi wa mpango huo ambao umewakutanisha vijana kutoka katika itikadi mbalimbali za vyama vya siasa.
“Nilipoambiwa hili jambo niliweka itikadi zangu za chama pembeni na kuuvaa Utanzania kwanza ili kuunganisha fani zetu wote kwa pamoja na kuweza kuwahimiza wananchi wadumishe amani tuliyokuwa nayo nchini” alisema Nyerere.
Aliongeza pia kwa kuwaomba viongozi wa dini masheikh na maaskofu wakiwemo mapadri wote kuungana nao wasanii hao katika kuhimizaani ya amani ya nchi.
“Sisi wasanii tunapata riziki zetu kutokana na amani na utulivu uliopo nchini mwetu hivyo kila msanii na Mmtanzania aone ni jambo la fedheha kuiichezea amani ambapo siku ikipitea tutakwenda kuomba hifadhi katika nchi za jirani zilizopata uhuru na kufuata ushauri kutoka kwetu”.,
Aliongeza kwa kusema kwamba ana imani kubwa watanzania watawaelewa pindi watakapokuwa katika ziara hiyo kuzunguka nchi nzima huku wakiwa na mabalozi watano kutoka kila nyanja ya sanaa ambazo ni muziki wa taarab, Hip Hop, Sanaa za maigizo, Michezo na tamthilia. Mkutano mkubwa unatarajiwa kufanyika Kibanda Maiti Zanzibar.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.