TANZANIA
YASISITIZA UWEZESHWAJI WA NCHI MASKINI
Na Mwandishi Maalum
Kikundi kazi cha Baraza Kuu
la Umoja wa Mataifa kilichopewa jukumu la kupendekeza Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015 ( SDGs) kimemaliza mkutano wake
wa kumi na moja kwa kupitisha maazimio mbalimbali.
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ni kati ya nchi 30 zinazounda kikundikazi hicho na imeendelea kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha kwamba, matakwa ya nchi maskini na zinazoendelea yanazingatiwa ipasavyo katika maandalizi ya malengo hayo mapya ambayo yatachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Millenia
( MDGs).
Wajumbe wa Kikundi kazi hicho walikutana kwa
wiki moja hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,
na kazi kubwa iliyofanyika katika wiki hiyo moja, ilikuwa ni kupitia na kuboresha rasimu ya malengo mapya ya maendeleo iliyokuwa imeandaliwa na Wawakilishi wa Kudumu wa
Kenya na Hungary ambao ni Wenyeviti -Wenza wa Kikundi Kazi hicho.
Rasimu hiyo ilijumuisha maeneo muhimu yaliyomo kwenye Malengo ya Millenia na ambayo yanahitaji msisitizo na msukumo zaidi katika mpango mpya wa maendeleo baada ya
2015. Maeneo hayo ni pamoja na kuondoa umaskni, kuhakikisha upatikanaji wa chakula,
afya, elimu na uwezeshaji wa wanawake.
Aidha maeneo mapya yanayojumuishwa ni pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama, nishati, miundombinu,
utunzaji wa mazingira yakiwamo ya baharini, kuhakikisha usawa miongoni na baina ya nchi,
na ujenzi wa jamii zenye amani, zinazo tingatia utawala bora
na utawala wa sheria
Akichangia majadiliano ya uboreshaji wa rasimi hiyo, Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania katikaUmoja wa Mataifa, na ambaye aliongoza ujumbe wa Tanzania
katika mkutano huo, alisisitiza umuhimu wa uwezeshaji makini wa nchi maskini na zinazoendelea.
Balozi Manongi alieleza kuwa nchi maskini na zinazoendelea zinapashwa kuwezeshwa ili kupitia uwezeshwaji huo basi ziweze kuwa katika nafasi nzuri ya kutekeleza malengo mapya ya maendeleo kama ilivyokubalika katika Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo Endelevu uliofanyika Rio de Janeiro, Brazil mwaka 2012.
Aliyataja maeneo ambayo nchi maskini na zinazoendelea zinahitaji uwezeshwaji makini kuwa ni pamoja na
, masuala ya biashara ambapo nchi zilizoendelea zinatakiwa kupunguza vikwazo vinavyozinyima nchi zinazoendelea kufaidi fursa za biashara ya kimataifa.
Vile vile Tanzania
imezitaka nchi zilizoendelea kuzisaidia nchi maskini kujenga uwezo wa kuendesha sekta muhimu kama
vile kilimo, uchukuzi, viwanda, elimu na afya, sekta ambazo Tanzania inaamini ni muhimu kwa maendeleo.
Katika mkutano huo wa kumi na moja na ambao pia Asasi zisizo za Kiserikali zilipata pia fursa ya kuwasilisha mapendekezo yao.
Tanzania pia imezitaka nchi zilizoendelea na zinazoibukia kiuchumi kuzipatia nchi maskini teknolojia salama na uelewa utakazo ziwezesha kuongeza kasi ya maendeleo nchi zao.
Balozi Manongi akiwasilisha maoni ya
Tanzania, pia alisisitiza suala la
upatikanaji wa fedha za ndani mathlani kupitia ukusanyajiwa mapato.
Pamoja na misaada na uwekezaji kutoka nje katika kufanikisha utekelezaji wa malengo hayo.
Kikundi kazi kinatarajiwa kuhitimisha shughuli zake Julai
2014 kwa kuwasilisha taarifa yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
ambaye naye ataiwasilisha taarifa hiyo kwenye Kikao cha 69 cha Baraza kuu la
Umoja wa Mataifa mwezi Septemba 2014.
Taarifa hiyo pamoja na taarifa za michakato mingine kuhusu
agenda ya maendeleo baada ya 2015,
itakuwa ndio msingi wa majadiliano ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa yatakayohitimishwa mwezi Septembea
2015 katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali ambapo wanatataraji wa kupitsha agenda
hiyo na malengo yamaendeleo endelevu ambayo ndiyo mrithi wa Malengo ya sasa ya Millenia.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.