Press Release
Wafanyakazi Airtel wachangisha fedha kwa ajili ya wanawake wanaougua kansa
UMOJA wa wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania unaofahamika kwa jina la Airtel Divas leo wameandaa halfa ya kuchangisha pesa kwa ajili yakina mama wanaosumbuliwa na maradhi ya kansa katika hospitali ya ocean road jijini Dar es salaam.
Halfa hiyo ya kuchangisha pesa ilifanyika katika makao makuu ya ofisi za Airtel Tanzania na kushirikiksha wafanya kazi wa Airtel Tanzania kwa ujumla
Akizungumza kwa niaba ya Airtel Ofisa Mahusiano na matukio Dangio Kaniki alisema” Airtel Tanzania kupitia Umoja wa wanawake Airtel Divas” tumeamua kuchangisha pesa kwaajili ya kina mama wenzetu ambao ni wagonjwa mahospitalini, ambapo leo tumeaandaa kifungua kinywa kwa wafanyakazi wote wa Airtel na kiasi cha pesa kitakachopatikana kitaenda kusaidia wanawake wanaougua ugonjwa wa kansa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Saalam.
Tunatambua jamii inayotuzunguka ina changamoto nyingi ikiwemo maradhi, na ndio sababu umoja wa wanawake wa Airtel tumeamua kuchangisha pesa kwa dhumuni la kuwasaidia wagonjwa hususani wakina mama wanaosumbuliwa na ugonjwa kansa. Tunaamini zoezi hili tunalolifanya leo litatuwezesha kufanikisha lengo letu. Mpango huu wa kusaidia jamii zinazotuzunguka ni endelevu, na tumejipanga kutoa misaada ili kuchangia katika kutatua vikwazo mbalimbali vya maisha na kujenga jamii iliyo bora. alisema Kaniki.
Kwa upande wa wafanyakazi Bi Doris Kibassa ambaye ni mmoja ya wanachama wa Airtel Diva alisema “ najisikia furaha kuwa sehemu ya kusaidia jamii, mbali na kampuni yetu kuwa na shughuli za kijamii bado sisi kama mfanyakazi tunanafasi ya kushiriki na kutoa msaada kwa jamii. Tunaamini mchango huu tunaoutoa leo utaweza kunusuru maisha ya baadhi ya watanzania na hivyo basi tunaziasa asasi nyingine kuiga mfano huu na kushiriki katika kuokoa maisha ya watanzania walio wengi,”
Airtel Tanzania imekuwa ikitoa michango kwa jamii kutupitia shughuli zake za huduma kwa jamii, Airtel kwa kushirikisha wafanyakazi wake pia inatoa huduma kwa jamii nchini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.