ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 12, 2014

KWANINI WANAWAKE HAWAPEANI NAFASI YA KUCHAGUANA LINAPOKUJA SUALA LA UONGOZI?

Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI Ramadhan Masele akiamsha mada katika Kongamano la kuleta Mabadiliko katika jamii lililokuwa likijadili Kwanini Wanawake hawapeani nafasi ya kuchaguana linapokuja suala la Uongozi? Kongamano lililofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Nyanza jijini Mwanza na kushirikisha wasomi wa vyuo mbalimbali vya jijini Mwanza, Wanaharakati na Wafanyakazi wa majumbani.
Mama Ana Chambo ambaye ni mmoja kati waanzilishi wa Shirika la kupambana na kuzuia ukatili wa kijinsia KIVULINI akitoa uzoefu wake kuhusiana na sababu alizobaini katika jamii  zinazopelekea Wanawake wengi kutopeana nafasi ya kuchaguana linapokuja suala la Uongozi. Ni katika Kongamano lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Nyanza jijini Mwanza na kushirikisha Wasomi toka vyuo mbalimbali, Wanaharakati na Wafanyakazi wa majumbani.
Taswira ya kusanyiko la kongamano.
Mratibu wa Kongamano hilo Bi. Khadija Liganga akiongoza taratibu mbalimbali ili kila mshiriki aweze kuchangia bila michango ya mawazo ya kujirudia rudia na humo ndani mengi yaliibuka.
Washiriki toka vyuoni.
Kwa umakini ndani ya Kongamano.
Wivu, kutopenda mafanikio na maendeleo ya mwanamke mwingine ni moja kati ya sababu zilizoanishwa na mshiriki Rosina Temalirwa kutoka chuo cha SAUT Mwanza.
Naye Faraja Dogeje toka Chuo cha SAUT Mwanza, alisema Tamaduni na mfumo wa maisha katika uongozi kuanzia kwenye jamii hadi mashuleni imekuwa ni sababu ya yote hayo. Nyumbani Dada ni mila kula jikoni akiwaacha wanaume sebuleni kujiachia, hata kwenye maamuzi baba ndiye mwenye kauli ya mwisho kwa familia nyingi. Shuleni nako Head Prefect anakauli zaidi ya Head Girly. Mifumo ambayo haimtayarishi mwanamke kuwa kiongozi.
 "Wanawake hatuthaminiani, wanawakewanadharau, ukimkuta kwenye ofisi fulani anafanya usaili hawezi kukuchagua iwapo kama ata gundua kuwa unasifa fulani za kushabihiana naye au zile unazomzidi ikiwa ni pamoja na muonekano wako" alisema Sophia Nestory Nshushi Mwanafunzi wa Sokoine University of Agriculture (S.U.A)
"Elimu ya kura inaonekana kama suala la kupoteza muda" alisema Joseph.
"Mfumo wa makuzi na malezi anayolelewa mtoto wa kike yanamjenga kutosimama mbele ya watu, na akisimama na kuzungumza anaonekana kama msemaji saaaana" "Dini nazo zinachangamoto zake" says Laurencia Mwilimu Igelegele Sec School.
 "Mbuzi huzaa watoto wawili kwa mwaka na mbwa huzaa watoto 12 kwa mwaka, mbuzi hulika kila siku mamia kwa maelfu nao mbwa hawaliki labda kwa kwa jamii ya wachache tu lakini linapokuja suala la SENSA kwa wanyama hao idadi ya mbuzi ni wengi kuliko mbwa kwanini? Tafakari" "Wanawake hawajiamini, hawajisimamii na hawajitambui" alisema Bartazar Bisansaba toka shirika la REHMMA.
"Vyombo vya habari haviwashape wanawake habari zao haziandikwi zaidi ya kuandikwa kwenye mapishi na shughuli za malezi pekee" alisema mama huyu.
Naye mtangazaji wa kipindi cha 'Wanawake Live' kinachoruka EATV Joyce Kiria alikuwa ni mmoja wa wawasilisha na wachangiaji mada ndani ya Kongamano hilo la kuleta Mabadiliko katika jamii lililokuwa likijadili Kwanini Wanawake hawapeani nafasi ya kuchaguana linapokuja suala la Uongozi? Kongamano lililofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Nyanza jijini Mwanza na kushirikisha wasomi wa vyuo mbalimbali vya jijini Mwanza, Wanaharakati na Wafanyakazi wa majumbani.

Mama Africa.
Big up KIVULINI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.