Toleo la Leo
SAFARI LAGER YATANGAZA RASMI BAA 5 ZILIZOINGIA FAINALI KATIKA SHINDANO LA UCHOMAJI NYAMA MKOA WA ARUSHA NA KILIMANJARO KWA MWAKA 2014.
Mwanza, Jumatano 12 Machi 2014: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi majina ya Bar 5 yaliyofanikiwa kuingia fainali katika shindano la uchomaji nyama kwa mwaka 2014 lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma Competition 2014”.
Shindano hili linalofanyika kila mwaka, linafanyika mwaka huu kwa mara ya saba mfululizo na litashirikisha mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Dar Es Salaam.
Tangu lilipoanzishwa mwaka 2008, shindano hili limekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya Safari Lager kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na ushindi katika mkoa waliopo.
Tangu lilipoanzishwa mwaka 2008, shindano hili limekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya Safari Lager kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na ushindi katika mkoa waliopo.
Kwa mwaka huu baa 5, zilizopigiwa kura kwa wingi(Top 5, Bars) –Arusha ni New City Garden,Royal Stop Over,Mile Stone Bar,QX Pub na Arusha Raha na kwa Mkoa wa Kilimanjaro ni East Africa Bar, Makanyaga Bar, White Star, Seven Eleven na Safari Forest.
Baa hizi zilizopata kura nyingi zaidi zitachuana kwa kuchoma nyama katika tamasha la wazi litakalofanyika katika Uwanja wa General Tyre ikisindikizwa na Bendi ya Yekete Bendi na kwa mkoa wa Kilimanjaro litafanyika katika Uwanja wa Grecious ikisindikizwa na Bendi ya Malindi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Kaskazini Chris Jo Salakana, alisema , “Lengo kuu la shindano la Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora katika uchomaji na utayarishaji wa nyama choma.
Tunahakikisha wachoma nyama katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma.
Alisema Fainali za Mashindano zitafanyika Machi 15 kwa Arusha na machi 16 kwa Kilimanjaro kuanzia saa tatu asubuhi.
Zawadi mshindi wa kwanza atapewa fedha taslimu Shilingi Milioni moja na Kikombe, mshindi wa pili Laki nane, Mshindi wa tatu Laki 6, Mshindi wa nne laki nne na Mshindi wa Tano shilingi laki mbili.
Bwana Chris alimaliza kwa kusema kwamba, “Safari Lager tutaendelea kujitahidi kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora ya nyama choma pale wanapoihitaji.
Tunawaomba sana washiriki kutumia vizuri elimu na uzoefu wanaopata ili kuongeza ubora wa utayarishaji wa nyama choma kwa wateja wetu.
Mashindano haya ya Safari Lager Nyama Choma yatakosa maana sahihi endapo wachoma nyama watakuwa wanashiriki kwa lengo la kujipatia manufaa binafsi na kusahau yale yote waliyojifunza hadi mwaka mwingine”. Shindano la mwaka huu linaongozwa na kibwagizo…. Bila Safari Lager, Nyama Choma haijakamilika!.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.