ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 10, 2014

VICTORIA PRINCE MABINGWA WA SAFARI NYAMA CHOMA 2014 MWANZA.

Mpishi Mkuu wa Victoria Prince Bar ,Godfrey Swai, ya jijini Mwanza akishangilia na Kikombe,cheti na pesa taslimu shilindi 1,000 000/= mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma 2014, mkoani humo yaliyofanyika katika Uwanja wa Furahisha mwshoni mwa wiki.Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Mpishi Mkuu wa Victoria Prince Bar,Godfrey Swai,  ya jijini Mwanza akishangilia na fedha taslimu Shilingi 1,000 000/= na cheti mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma 2014, mkoani humo yaliyofanyika katika Uwanja wa Furahisha mwshoni mwa wiki. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo,Meneja matukio wa TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela(kushoto).
Mshindi wa pili katika fainali hizo ni Gemestone Bar ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi laki nane (800,000/=),
Mshindi wa tatu ni SD Executive Bar ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki sita (600,000/=), 
Mshindi wan nne ni Shooters Pub ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki nne (400,000/=)
Nyama choma mezani.
Akionyesha mautundu ni tumba boy wa bendi ya Sebedaki ya jijini Mwanza .
Mwimbaji wa Alle Totapak aka Rais wa Freemasons.
Mikogo na manjonjo ya Alle Totapak.
Bass gitaa.
Full madoido.
Nakshi za hapa na pale.
Mmoja kati ya wadau wa baa shiriki katika shindano la Safari Lager Nyama choma 2014 akiwa kazini.
Wadau wa ukweli wa Mwanza Kwanza walipozi hapa.
Chief judge akionyesha jinsi ukaguzi wa nyama iliyoiva unavyofanyika.
Kipimo kwa ukaribu zaidi.
Samaki choma nazo zilikuwepo.
Sauti adimu zikishambulia jukwaa kutoka kwa Allen Totapak (kushoto) na Zarri (kulia)
Wadau wa TBL Mwanza wakigonga stori huku wakimimina mimina.
Mwimbaji Allen Totapak akichombeza vipande vya rap huku madensa wa Sebedaki Band wakijiachia katika tukio lililofanyika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
Chief judge akiendelea kufanya ukaguzi wa nyama choma.

Wadau wangu na meza yetu.
Ma-densa wa Sebedaki Band wakilishambulia jukwaa.
Victoria Prince Mwanza Mabingwa Safari Nyama Choma 2014.
VICTORIA PRINCE BAR wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2014 yaliyofanyiaka mswishoni mwa wiki katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja(1,000 000/=) na Kikombe.

Mshindi wa pili katika fainali hizo ni Gemestone Bar ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi laki nane (800,000/=), mshindi wa tatu ni SD Executive Bar ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki sita (600,000/=), mshindi wan nne ni Shooters Pub ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki nne (400,000/=) na nafasi ya tano ilichukuliwa na Lunala Bara ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki mbili (200,000/=)

Akizungumza na wakazi jiji la Mwanza waliohudhuria fainali hizo, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Bi. Amina Masenza  aliwashukuru kampuni ya bia Tanzania(TBL) kwa kuanzisha mashindano hayo yenye mvuto wa pekee na yenye kutoa ajira na kukuza kipato kwa wachoma nyama na si hilo tu hawa walianza kwa semina malumu ya mafunza hivyo Serikali inaamini wanazingatia taratibu zote za afya kwa kuandaa nyama inyokidhi viwango kwa mlaji.

Pili aliwapongeza baa tano zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika baa zote zinazochoma nyama mkoani humo na aliwaomba waendelee kuilinda hadhi na sifa hiyo waliyopewa katika jiji la Mwanza na mwisho aliwapongeza mabingwa wa Victoria Prince kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2014 na kuwaomba ambao hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo wajiandae kwa mashindano yajayo ya Safari Nyama Choma 2015.

Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2014, Victoria Prince na pia aliwashukuru wote walioshiriki toka mchakato ulipoanza mpaka kufikia kumpata bingwa lakini pia aliwashukuru wakazi wa Mwanza waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia nani anatwaa ubingwa mwaka huu.

Mwisho shelukindo aliwaomba wakatumie vyema zawadi walizopata kwa kuboresha majiko yao kwa mashndano yajayo ya 2015.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.