Waibaji na wacheza show wa Bebdi ya Kakao wakitumbuiza kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo kipya cha MSD eneo la Mahalahala Muleba. |
Viongozi Jukwa Kuu wakishiriki kusakata rumba la Kakao Bandi |
Afisa Habari wa MSD Makao Makuu (Mwenye Kipeperushi cha Bendera ya MSD) na Baadhi ya watumishi wakifuatilia kwa umakini shughuli za uzinduzi wa Kituo kipya |
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa nchini (MSD) akitoa taarifa fupi ya MSD kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo kipya. |
Zamu ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Prof. Idris Alli Mtulia akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Kituo hicho. |
Baadhi ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali ya uzinduzi wa kituo kipya cha MSD Muleba. |
Kakao Bandi wakiwa kazini kutumbuiza wakati wa sherehe |
Baadhi ya wanawake wakifuatilia tukio la uzinduzi |
Kazi ni moja tu kushambulia ndani ya viwanja vya uzinduzi wanamuziki wa Kakao Bandi. |
"Haya tupige makofi kwa pamoja kuashiria kukubali uzinduzi huu" Naibu Waziri Dk. Kebwe (Kulia), Waziri Prof. Tibaijuka (Katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu MSD Bw. Mwaifwani |
Na Peter Fabian.
ALIYEKUWA MULEBA.
MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
Mohamed Gharib Bilal ameiagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kushirikiana
na Jeshi la Polisi nchini kufanya msako endelevu ili kuwafichua, kuwakamata na
kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaopatikana na Dawa za Serikali
kinyume cha taratibu na sheria zilizopo.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Stephen Kebwe (MB) wakati
wa ufunguzi rasmi wa Kituo cha Kutunza na Usambazaji Dawa (Bohari ya MSD) cha
muda kilichopo eneo la Mahalahala kwenye Hospitali inayojengwa ya Wilayani
Muleba juzi alisema wizi na upotevu wa dawa hizo zinazotolewa na serikali hufanywa
na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.
Alieleza kwamba Kituo cha Muleba (Bohari ya Madawa
ya MSD) cha muda kitakuwa na jukumu kubwa la kusambza dawa na vifaa tiba kwa
ajili ya Hospitali na Vituo vya Afya katika maeneo yote ya Wilaya za Mikoa ya
Kagera (Vituo 270 ) na Geita (Vituo 64) kuanzia mwezi julai mwaka 2013 mfumo
huu wa usambazaji dawa ulianza kabla ya kufunguliwa rasmi.
Makamu wa Rais Dk. Katika hotuba hiyo ameipongeza Bohari
Kuu ya Madawa (MSD) nchini kwa kuanzisha utaratibu wa kuweka alama ya Government
Of Tanzania (GOT) katika dawa zinazosambazwa na kusema kuwa hatua hiyo
itasaidia dawa za serikali kutambulika kiurahisi kwa wananchi pamoja na
kuthibiti wauzaji wa maduka ya dawa baridi wanaopelekewa zinazoibiwa na
watumishi wa serikali.
“Lengo kubwa la kufunguliwa kituo hichi ni kupunguza
vifo vya akina mama na watoto, kupambana na ungonjwa wa UKIMWI na Malaria ikiwa
ni kuanza kutumia mfumo wa fikisha dawa karibu na wananchi na kwa wakati ili
kufanikisha lengo mahususi la serikali ya awamu ya nne huku ufatiliaji wake uwe
chini ya usimamizi wa karibu na matumizi ya dawa zinazosambazwa kwenye vituo
vya huduma ” alisisitza
Kwa upande wake Naibu Waziri Dk. Kebwe amesikitishwa
na taarifa ya kasi ya wizi na upotevu wa dawa zinazopelekwa na serikali kupitia
Bohari ya Dawa (MSD) katika Wilaya za Ngara, Kerwa, Biharamulo na Muleba huku
akizipongeza Wilaya za Karagwe na Bukoba vijijini kwa kuweka jukumu la udhibiti
wizi na upotevo wa dawa hizo kutoka kwa watumishi wasio waadilifu.
Dk. Kebwe ameungana na Makamu wa Rais Dk. Bilal
kuzitaka Kamati za ulinzi na usalama za Mikoa ya Kagera na Geita na zile za Wilaya
kwa kushirikiana na Wakurugenzi na Wenyeviti wa Halmashauri zote kufatilia kwa
ukaribu huku akitaka taarifa za upokeaji dawa na utolewaji kwa wananchi utolewe
kwenye Vikao vya Kamati ya Ushauri na Maendeleo (RCC) za Mikoa yote.
“Tusikubaliane na wajanja wachache wa Idara za Afya
kutumia mwanya wa kuiba dawa na kuziuza kwenye maduka waliyoanzisha na kisha
kujinufaisha kwa kununua magari, kujenga vyumba za kifahari nasi kuwashangilia
eti muda mchache jamaa ana gari zuri ambapo makusanyo ya mapato kutoka vituo
vya afya kuonyesha ni asilimia 50 tu huku zingine zikiliwa na wajanja wachache”
alisema.
Dk. Kabwe alisema kuwa Wizara yake itatumia bilioni
6 kwa mwaka katika Dawa zote zitakazotolewa na kituo hicho na kila mwezi
kitasambaza dawa za kiasi cha shilingi milioni 150 huku Bajeti ya Wizara
ikionekana kutumia Bilioni 80 za Dawa, Vifaa tiba na Vitenganifu na kupitia
kituo hicho ndani ya siku 14 Hospitali na Vituo vya Afya vitapeka oda na
kupatiwa dawa.
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Porfesa
Idrisa Mtulia kuzinduliwa kwa kituo hicho ni mkombozi mkubwa wa wananchi wa Mkoa
ya Kagera na Mkoa wa jirani wa Geita na Wilaya zake zote ambapo kitawezesha
upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na viunganifu vya kutolea huduma ya afya kwa
Bohari ya madawa kufikisha haraka huduma zake kwa wateja.
Prof. Mtulia alisema kwamba pamoja na changamoto
mbalimbali zinazoikabili MSD itahakikisha inashirikiana na serikali na wadau
wengine kuendelea kutoa huduma bora na kufikisha dawa zenye ubora na bei nafuu
wakati wote kwa manufaa ya watanzania wote
huku akihimiza Halmashauri zote nchini kukunua dawa kutoka MSD kwa
kutumia vyanzo vyake vingine vya fedha.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu
ya Dawa (MSD) nchini Cosmas Mwaifwani alisema kwamba kutokana na ukubwa wa
Kanda ya Ziwa na idadi kubwa ya wingi wa watu zaidi ya milioni 13 kutokana na
matokeo ya Sensa ya mwaka 2012 kuwepo na malalamiko ya wadau mbalimbali juu ya
huduma za MSD Kanda ya Mwanza kutokidhi kwa wakati huduma ya utoaji wa dawa.
Kaimu huyo alieleza kuwa imefungua kituo hicho cha
muda kuhakikisha upatikanaji na usambazaji wa Kituo cha Muleba kinafanikisha
lengo la MSD na kupunguza usumbufu wa Mkoa wa Kagera kufata huduma hiyo Jijini
Mwanza na Kanda ya Tabora ambapo ilionekana kuchelewesha upatikanaji wa dawa,
vifaa tiba vyenye ubora na kwa bei nafuu kwa watanzania wote.
“Ufunguzi
wa Kituo hiki cha usambazaji dawa Mkoani Kagera na Mkoa wa jirani wa Geita ni
mchango mkubwa wa utekelezwaji wa Malengo ya Millenia hususani kupunguza vifo vya
mama na watoto na kupambana na Ukimwi na Malaria ambayo imekuwa ni magonjwa ya
mlipuko katika maeneo mengi ya Wilaya za Muleba ” Alisema Mwaifwani.
Mbunge wa Muleba Kusini Porfesa Anna Tibaijuka
ambaye ni Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwahakishia
Naibu Waziri Dk. Kebwe na uongozi wa MSD kuwa eneo la Ekhali 5 zilizotolewa na
Halmashauri Wilaya ya Muleba linaachwa wazi ili kutoa nafasi kwa MSD kujenga
Ofisi kuu na Maghala ya kuhifadhiwa dawa Mkoani humo.
“Kituo hiki ni wajibu wetu kukilinda na kukitunza
vizuri ili kiendelee kutoa huduma, lakini Mkurugenzi wa Halmashauri naomba utumia
sheria za ardhi zilizopo kuhakikisha unawaondosha watu wanaovamia eneo
tulilotenga kwa ajili ya shughuli za MSD hili ni agizo natoa kama Waziri nila
serikali siyo langu kama Mbunge wa Jimbo hili” alisisitiza.
Mbunge huyo aliongeza kuwa kutokana na waathilika
wakubwa ni Kimama na watoto pamoja na Wilaya hiyo kukubwa na magojwa ya mlipuko
hususani Malaria ambayo yalipelekea serikali na Wizara ya Afya kutuma wataalamu
na kufanya utafiti kisha kuanzisha mkakati wa kupulizia dawa ya Ukoko kwenye
nyumba za Wilayah ii ili kudhibiti ugonjwa huo uliokuwa ni janga kwa wananchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.