Kwa umakiiini huku wakichukuwa maelezo muhimu mafunzoni. |
Washiriki toka baa mbalimbali za jijini Mwanza wako hapa. |
Rejina Mussa Sakara yeye si mshiriki toka bar yoyote jijini Mwanza, bali ni mshiriki toka nyumbani, anasema ameshiriki semina ya Safari Lager Nyama Choma kwaajili ya kuboresha ndoa yake kwa kujijengea uwezo kumpikia mumuwe. |
Wanasemina seminani. |
Wachoma Nyama wapigwa msasa - Mwanza
KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL)
kupitia kinywaji chake cha Safari Lager jana imetoa mafunzo kwa wachoma
nyama kutoka Baa mbali mbali za Mkoa wa Mwanza ikiwa ni maandalizi ya
mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2014 yatakayo fanyika katika viwanja
vya Furahisha.
Akizungumza na waandishi wa
habari, Meneja matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kanda ya Ziwa, Erick
Mwayela, alisema lengo la kutoa mafunzo ni kutoa elimu kwa wachoma nyama
ukizingatia uchomaji nyama ni moja sehemu ya kujiingizia kipato katika
Bar.
Mwayela alisema kutokana na
hali hiyo wakaona ni vema wakaendesha Semina kwa wachoma nyama ili waweze
kukidhi vigezo vya mahitaji ya Wateja ili waweze kufurahia Nyama choma kama
ilivyo kwa vyakula vingine ili kuendana na kauli Mbiu ya Bia ya Safari Lager
isemayo“ Safari Lager bila nyama choma haijakamilika.”
Aliongeza kuwa baada ya
mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Baa 37 ambao wametunukiwa vyeti vya
ushiriki pia kutakuwa na mashindano ya kuchoma nyama ambapo washindi 10
watapatikana kutokana na watakaofuzu vigezo na masharti waliyopewa katika
semina hiyo.
Alisema Fainali za Mashindano
zitafanyika Machi 9, Mwaka huu katika Viwanja vya Furahisha ambapo washindi
watapewa zawadi kuanzia mshindi wa kwanza atakayejinyakulia Shilingi Milioni
moja na Kikombe, mshindi wa pili Laki nane, Mshindi wa tatu Laki 6, Mshindi wa
nne laki nne na Mshindi wa Tano shilingi laki mbili huku mshindi wa Sita hadi
wa Kumi watajinyakulia kifuta jasho cha shilingi 50,000/=.
Alisema namna ya kuwapata washindi ni kutokana na wateja kupiga
kura katika utaratibu utakaobandikwa katika Baa shiriki ambapo mteja atapiga
kura kupitia simu ya mkononi ili kuichagua baa inayochoma nyama vizuri.
Aliongeza kuwa baada ya zoezi
hilo kukamilika katika Mkoa wa Mwanza itaendelea katika Mikoa mingine ambayo ni
Kilimanjaro,Arusha na Dar Es Salaam, mikoa ambayo imetajwa kuwa ndiyo vinara wa
uchomaji nyama pamoja na kuongoza kwa mauzo ya bia ya Safari Lager tofauti na
maeneo mengine.
Kwa upande wake Mkufunzi wa
Mafunzo hayo, Laurence Salvi ambaye pia ni Jaji Mkuu wa mashindano hayo
amesema huwezi kuandaa mashindano bila ya kutoa Elimu, hivyo TBL wamefikiria
jambo la msingi sana lenye manufaa kwa waandaaji yaani wachoma nyama mpaka kwa
watumiani yaani mlaji.
Bwana Lawrence binfsi
aliishukuru TBL kupitia bia ya Safari Lager kufikiria jambo zuri la kufadhili
elimu kwa kwa wachoma nyama jambo ambalo si faida kwa wachoma nyama tu bali
hata watumiaji sasa watakula nyama inayostahili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.