ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 19, 2014

NGUVU YA MCHEZO WA BAO KATIKA JAMII YETU.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani jijini Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akikabidhi zawadi ya mbuzi kwa  nahodha wa washindi wa pili wa mashindano ya mchezo wa draft wilaya ya Nyamagana timu ya Mmarekani, katika fainali ya michezo iliochezwa katika viunga vya Mkolani Centre ambapo jumla ya timu 9 zikitoka kata za jirani za Butimba na Buhongwa zilishiriki lengo la mashindano ni kuvumbua vipaji vya mchezo wa draft, kujuana na kukuza mahusiano baina ya wananchi wa kata mbalimbali wilayani Nyamagana. 
Awali katika kuonyesha kipaji chake na kwamba mchezo anaufahamu vyema,  Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani jijini Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula alipata nafasi kucheza draft katika mechi ya ufunguzi. 
Macho kwenye mchezo.
Sasa ni nusu fainali timu mbalimbali zikichuana kwa mtindo wa ligi. 
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akizungumza na wadau wamchezo huo alibainisha kuwa michezo ni sehemu ya kuchangamsha akili, kujadili chagamoto za jamii, kutengeneza urafiki (kuboresha mahusiano), kufungua fursa kwa kutambuana vipaji na sifa za kila mmoja kwa njia mazungumzo mchezoni, vilevile mchezo huo kwa wazee wenye busara wanaweza kuutumia kuwajengea vijana wao kuwapa uwezo kimawazo ili wawe na upeo wa kufikiri na kutanzua changamoto zao ikiwa ni pamoja na kujiepusha na maovu.
Sehemu ya wadau waliohudhuria michuano ya mashindano ya mchezo wa draft ambapo timu washindi wa kwanza na wa pili walizawadiwa mbuzi mnyama kila mmoja.  Timu ya Balekele ndiyo ilichukuwa ubingwa na wa pili ni timu ya Mmarekani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.