Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mary Tesha akitaka maelekezo kutoka kwenye kabrasha la Kikao hicho (Kulia) na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Magu Jackiline Liana na Mkuu wa Wilaya Ilemela Amina Masenza |
Sehemu ya Wajumbe ambao ni Wabunge wa Majimbo ya Mkoa wa Mwanza |
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Hassan Hida |
Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor akitaka ufafanuzi juu ya ujenzi wa kiwango cha lami kutoka Hungumalwa kupitia Mwankurwe, Nyamilama, Ngudu hadi Magu. |
Meneja wa TANROAD Mkoa wa Mwanza Eng. Leonard Kadashi akitoa ufafanuzi wa hoja za wajumbe wa kikao hicho kinachoendelea sasa. |
Mwenyekiti wa Kikao Eng. Evarist Ndikilo (Mkuu wa Mkoa wa Mwanza) akisisitiza jambo kwenye kikao. |
Ndani ya Kikao Ukumbi wa BOT Mwanza. |
Akizungumza katika kikao cha Bodi hiyo kilihofanyika leo kwenye chuo cha Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kapiripoint jijini hapa, Mwenyekiti wa kikao hicho, mhandisi Evarist Ndikilo ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, ameagiza Meneja huyo ‘alimwe’ barua ya onyo na nakala yake apewe Waziri wa Ujenzi.
Ndikilo alisema kwamba, Meneja huyo ameshindwa kutekeleza maazimio ya kikao kilichopita cha Bodi hiyo kwa muda wa mwaka mzima sasa na kukacha kikao cha jana bila majibu sahihi ya utekelezaji, hali inayoonyesha amekidharau kikao hicho.
Aliyataja maagizo hayo kuwa ni kuweka choo katika kivuko cha MV Kome II kinachotoa huduma kati ya Nyakarilo na kisiwani Kome wilayani Sengerema na kutoa elimu ya matumizi ya vifaa vya kujikololea kwa abiria wa vivuko vyake vyote mkoani humo.
Agizo jingine ni kuwanunulia sare wafanyakazi wa vivuko hivyo ambao inadaiwa wengi wao wamezigomea baada ya kutakiwa wakatwe gharama ya sare hizo kwenye mishahara yao.
“Temesa wamedharau agizo la Bodi hii tulilolitoa mwaka mzima uliopita, Meneja wake aandikiwe barua ya onyo na RAS na kutakiwa kutoa majibu ya utekelezaji wa maagizo hayo katika kikao kijacho.” Alichachamaa Ndikilo na kuagiza nakala ya barua hiyo ya onyo ipelekwe kwa Waziri wake wa Ujenzi, John Mgufuli.
Hatua hiyo ilitokana na Kaimu Meneja wa Temesa Dauson Nyonyi kushindwa kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu utekelezaji wa maagizo hayo alipoeleza kuwa, mkandarasi hajaweka choo hicho katika kivuko cha Kome II liha ya kutakiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka jana.
Nyonyi alisema, TEMESA imeweka kanda za CD katika vivuko vyake ambazo zinaonyesha namna ya kutumia vifaa vya kujiokolea vikiwemo Life Jacket na kuwanunulia sare wafanyakazi wa vivuko vyake vyote bila lakini baadhi ya wajumbe walikataa kuwa taarifa hiyo ya TEMESA si sahihi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Buchosa ndiye aliyeanza kupinga utekelezaji wa maagizo hayo alipodai kuwa mkandarasi Songoro Marine Transport, toka mwaka jana ametengeneza choo hicho lakini hadi sasa Meneja wa TEMESA hataenda kukihukua na hana mawasiliano na Songoro.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, Joseph Mkundi, alisema majibu ya Nyoni si sahihi kwani sare hizo zimenunuliwa lakini hazijagawiwa kwa wafanyakazi kutokana na kutakiwa kukatwa garama ya nguo hizo katika mishahara yao na hivyo kuwafanya wazisusie.
Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Karen Yunus alikiambia kikao hicho kwamba, TEMESA ni waongo, hawajatoa mafunzo yoyote ya matumizi ya vifaa vya kujiokolea kwa wateja wao (abiria) na hawajawapa sare huku akisisitiza kuwa wanapaswa kupewa sare hizo bila kukatwa katika mishahara yao.
Pamoja na michango ya wajumbe wengine, kikao hicho kilikataa majibu ya TEMESA na kudai kuwa ni blablaa tu kinataka kuona utekelezaji kwa vitendo na pamoja na kumpa onyo Senkoro, kilimuagiza atekeleze haraka maagizo hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.